Pata taarifa kuu
MEXICO-Haki za binadamu-Usalama

Wanafunzi waliotoweka Mexico: hasira zaongezeka

Maandamano, baadhi ya amani, na mengine kukumbwa na machafuko yametokea Jumatano Novemba 12 katika majimbo mbalimbali ya Mexico.

Majengo ya wizara ya elimu yalichomwa moto katika mji wa Chilpancingo, Novemba 12 mwaka 2014.
Majengo ya wizara ya elimu yalichomwa moto katika mji wa Chilpancingo, Novemba 12 mwaka 2014. REUTERS/Jorge Dan Lopez
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji wameendelea kuomba kurejeshwa wakiwa hai waanafunzi 43 waliyotoweka katika mji wa Iguala. Lakini maandamano yenye vurugu yanaonekana kushika kasi katika mji mkuu wa Guerrero, Chilpancingo. Mamia ya wahadhiri kwenye chuo cha Iguala walishambulia majengo ya serikali, ikiwa ni pamoja na jengo la Bunge la kikanda.

Raia kutoka maeneo mbalimbali ya Mexico wamekua wakiandamana tangu walipotoweka wanafunzi 43, wakidai warejeshwe wakiwa hai. Hata hivo hivi karibuni viongozi wa Mexico walithibitisha kwamba wanafunzi hao waliuawa na genge la wahuni, kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi wa mji wa Iguala na askari polisi.

Mwanzoni mwa wiki hii, wataalamu kutoka Argentina waliokua katika timu ya uchunguzi wa miili ya watu iliyogunduliwa katika kaburi moja, walithibitisha kwamba kulingana na uchunguzi waliyoendesha, imedhihirika kuwa miili hiyo sio ya wanafunzi 43 waliotoweka hivi karibuni.

Wahadhiri hao wamekua na hasira hadi kuchoma moto magari na majengo ya serikali katika mji wa Guerrero. Jengo la Bunge na maktaba viliteketea kwa moto.

Kulingana na uchunguzi uliyoendeshwa na wataalamu kutoka Argentina, wazazi wa wanafunzi hao 43 bado wana imani kuwa watoto zao wako hai.

Jumanne Novemba 11, makao makuu ya chama tawala cha PRI yalichomwa moto na waandamanaji, huku vizuizi vikiwekwa kwenye baadhi ya barabara za mji wa Guerrero.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.