Pata taarifa kuu
MEXICO-Haki za binadamu-Usalama

Mexico: Raia wamtaka Peña Nieto ajiuzulu

Maelfu kwa mamaia ya raia wa Mexico waliandamana kwa mara nyingine tangu Jumamosi na jumapili Novemba 9 ili kudhihirisha hasira yao baada ya Mwendesha masktaka mkuu kutangaza vifo vya wanafunzi 43 wa vyuo vikuu waliokosekana katika mji wa Igula.

Mmoja wa waandamanaji akihamisha vizuizi  mbele ya Ikulu, Mexico, Novemba 8 mwaka 2014.
Mmoja wa waandamanaji akihamisha vizuizi mbele ya Ikulu, Mexico, Novemba 8 mwaka 2014. REUTERS/Edgard Garrido
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji hao walichoma mlango wa kuingilia Ikulu. Baadhi ya raia wa Mexico wamemtaka rais wa taifa hilo, Peña Nieto, pamoja na mwendesha mashtaka anafuatilia kesi ya wanafuzi hao wajiuzulu.

Wakti wa mkutano na waandishi wa habari, Mwendesha mashtaka mkuu alitangaza Ijumaa Novemba 7 kwamba wanafuzi 43 waliokosekana katika miezi ya hivi karibu katika mji wa Iguala wanasadikiwa kuwa walifariki,

Baadhi ya mandamano ambayo yalitokea mwishoni mwa wiki hii yalendelea kuenea nchi nzima. Katika mji mkuu wa jimbo la Guerrero, Chilpancingo, , wanafunzi wa vyuo vikuu walishambulia makao makuu ya serikali ya mkoa.

Wakati huohuo maandamano ya amani yalishuhudiwa katika mji wa Mexico Jumamosi huku kukiripitiwa visa vya uharibifu. Waandamanaji ishirini, ambao baadhi yao walificha nyuso zao, walichoma moto mlango mkuu wa kuingilia ikulu bila hata hivo kuingia katika jengo hilo la kihistoria.

Maandamano mengi ya mwishoni mwa wiki hii yaligubikwa na hasira, huzuni, na kukadi amri za serikali.

Maefu ya waandamanaji wamekua wakiomba mwishoni mwa juma liliyopita kurejeshwa kwa wanafunzi hao. Waandamanaji hao hawakukubaliana na kauli ya Mwendesha mashtaka mkuu ya kusema kwamba wanafunzi waliuawa na miili yao kuchomwa moto.

Hivi karibuni kundi la wahuni nchini Mexico lilikiri kuwaua wanafunzi hao na baadaye kuchoma kwa moto miili yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.