Pata taarifa kuu
MEXICO-Haki za binadamu-Usalama

Mexico: miili iliyogunduliwa sio ya wanafunzi waliotoweka

Wazazi wa wanafunzi waliotoweka nchini mexico wamekutana kwa mara nyingine tena Jumanne Novemba 11 na viongozi wa Mexico.

Wazazi, ndugu na jamaa wa wanafunzi 43 waliotoeweka, wakitokea mkutanoni na viongozi wa Mexico, Jumatatu Novemba mwaka 2014.
Wazazi, ndugu na jamaa wa wanafunzi 43 waliotoeweka, wakitokea mkutanoni na viongozi wa Mexico, Jumatatu Novemba mwaka 2014. REUTERS/Daniel Becerril
Matangazo ya kibiashara

Lengo la mkutano huo ilikua kujua maendeleo ya uchunguzi unaolenga kujua wapi walipo wanafunzi hao wa chuo kikuu cha Ayotzinapa, ambao hawajulikana walipo tangu mwezi mooja na nusu uliyopita.

Wakati huo wazazi wa wanafunzi hao walifahamishwa na madaktari kutoka Argentina kwamba miili iliyogunduliwa hivi karibuni katika makaburi ya pamoja karibu na mji wa Iguala, si miili ya wanafunzi wanaotafutwa.

Wazazi wa wanafunzi hao waliotoweka wamekata tamaa ya kuwapata watoto zao, baada ya kuthibitishiwa na madaktari hao kutoka Argentina ambao walikua wakifanya uchunguzi wa vipimo vya damu kwa miili ya watu iliyogunduliwa hivi karibuni katika makaburi ya pamoja karibu na mji wa Iguala. Hata hivo baadhi ya wazazi wamekua na imani kuwa watoto zao bado wako hai.

Maandamano na vurugu vilishuhudiwa Jumanne Novemba 11 katika mji mkuu wa jimbo la Guerrero, saa kadhaa kabla ya mkutano huo uliyofanyika katika mji wa Chilpancingo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.