Pata taarifa kuu
UNSC-GAZA-ISRAELI-HAMAS-Mapigano

UNSC yaitaka Israeli na Hamas kusitisha mapigano

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeelezea kuguswa na mapigano yanayoendelea huko Gaza na kusisitiza wito wa kusitishwa mapigano kwa Israel na Hamas kutii sheria ya kimataifa ya haki za binadamu, wakati huu kukiripotiwa uhitaji mkubwa wa huduma za kibinadamu huko palestina kwa wahanga wa vita.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa waitaka israeli na Hamas kusitisha mapigano haraka iwezekanavyo bila masharti.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa waitaka israeli na Hamas kusitisha mapigano haraka iwezekanavyo bila masharti.
Matangazo ya kibiashara

Mataifa 15 wanamemba wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yaliyofanua mktano wa dharura, yametangaza kuunga mkono makubaliano ya kusitisha mapigano haraka iwezekanavyo bila masharti, ili misaada iweze kuwafikiya walengwa.

Mataifa hayo yameitaka Israel na Hamas kutekeleza makaubaliano ya kusitisha mapigano kwa kipindi chote cha siku kuu ya Aïd el-Fitr ambayo inashiriya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, na vile vile kuheshimu makubaliano hayo na baada ya siku kuu hiyo.

kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. REUTERS/Eduardo Munoz

Mkutano wa baraza la usalama unakuja baada ya rais wa Marekani Barack Obama kutoa wito wa kusitishwa mapigano mara moja yanayoendelea huko Gaza baada ya israel na wapiganaji wa Hamas kutotilia maanani hatua hiyo na kuchochea makabiliano kuingia wiki ya tatu jumatatu hii.

Rais wa Marekani, Barack Obama.
Rais wa Marekani, Barack Obama. REUTERS/Kevin Lamarque

Rais Obama alizungumza na waziri mkuu wa israel Benjamin Netanyahu kwa njia ya simu jumapili na kumueleza wazi mpango wa kutekelezwa mara moja kusitishwa kwa mapigano bila masharti yoyote kwa kujali ubinadamu na kukomesha ukatili sasa kwa kuzingatia makubaliano yaliyowahi kufikiwa mwezi Novemba 2012.

Kwa upande wao kundi la hamas limepinga maneno yanayotolewa na israel.

Hakuna kombora liliyorushwa kutoka kwenye aridhi ya Gaza, hata Israel haijafanya mashambulizi yoyote katika ukanda wa Gaza toka saa mbili usiku saa za kimataifa, msemaji wa jeshi la Israel amethibitisha.

Kwa mujibu wa mashrika yanayotoa huduma za uokozi, wapalestina 1.030 wameuawa tangu mapigano hayo yalipoanza. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, miongoni mwa watu wanne wanaouawa, watatu ni raia wa kawaida.

Kwa upande mwengine wanajewshi 43 wa Israel tangu jeshi la Israel lilipoanzisha mashambulizi ya anga katika ukanda wa Gaza, Julai 17.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.