Pata taarifa kuu
ECUADO-MAREKANI-URUSI-CHINA

Ecuador yasema Urusi ndio inapaswa kuamua juu ya hatma ya hifadhi ya Edward Snowden

Rais wa Ecuador Rafael Correa amesema Urusi ndiyo inayopaswa kuwa na uamuzi wa mwisho juu ya kumpatia hifadhi ya kisiasa mfanyakazi wa zamani wa shirika la kijasusi duniani la nchini Marekani CIA Edward Snowden ambaye mpaka sasa ameendelea kusalia mjini Moscow.

REUTERS/Courtesy of The Guardian/Glenn Greenwald/Laura Poitras
Matangazo ya kibiashara

Rais Correa amesema kwa sasa Ecuador haina mamlaka ya kumpatia hifadhi Snowden kwani yupo katika nchi nyingine, kwa mujibu wa Correa nchi hiyo ingefikiria ombi la kumpatia hifadhi Snowden endapo angekuwa ndani ya mipaka ya nchi hiyo.

Mapema juma hili Ecuador ilisema ipo katika mchakato wa kuangalia iwapo uamuzi wa kumpatia hifadhi Snowden hautavunja sheria za kimataifa.

Marekani na Ecuador imekuwa katika majibizano juu ya swala la Bwana Snowden wakati huo huo Marekani imekuwa ikiishutumu Urusi na China kwa kushindwa kumkabidhi Snowden.

Snowden anatuhumiwa kuvujisha siri za ndani za Marekani na hivi sasa bado yupo katika uwanja wa ndege mjini Moscow toka alipowasili nchini Urusi jumapili iliyopita akitokea mjini Hong Kong nchini China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.