Pata taarifa kuu
VENEZUELA

Henrique Capriles kupambana na Nicolas Maduro katika kuwania Urais wa Venezuela

Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Henrique Carpiles ametangaza kugombea urais wa nchi hiyo kwa mara nyingine tena akiwania kuziba pengo lililoachwa na marehemu Hugo Chavez aliyefariki dunia juma lililopita baada ya kukabiliwa na maradhi ya saratani kwa takribani miaka miwili.

REUTERS/Carlos Garcia Rawlins
Matangazo ya kibiashara

Rais wa muda wa Taifa hilo Nicolas Maduro ambaye naye anayewania kiti hicho atapambana na Capriles mwenye umri wa miaka 40 ambaye ni Gavana katika mji wa Miranda.

Capriles ambaye aliangushwa na Chavez katika uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba mwaka jana baada ya kutangaza uamuzi wake amewashutumu viongozi wa nchi hiyo kwa kutumia kifo cha kiongozi wao kama mtaji wa kisiasa.

Capriles amemshutumu mpinzani wake Maduro kuwa ni muongo kwani alidanganya umma kuhusiana na kifo cha Chavez.

Kura za maoni za hivi karibuni zinampa Maduro umaarufu wa pointi 14 zaidi ya Capriles.

Kabla ya kifo chake Chavez alikuwa akishutumiwa na wapinzani kwa kutumia madaraka isivyotakiwa sambamba na kuendesha kampeni zake za uchaguzi kwa kutumia fedha za fedha za serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.