Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KUSINI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Visa vipya vya maambukizi vyaongezeka Korea Kusini

Korea Kusini imetangaza kwamba visa vya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 vimeongeze, baada ya kupungua kwa visa vilivyothibitishwa siku kadhaa zilizopita.

Maafisa wa afya nchini Korea Kusini wanaendelea na mapambano dhidi ya kuenea kwa virusi vya Covid-19 katika huko Seoul, Machi 12, 2020.
Maafisa wa afya nchini Korea Kusini wanaendelea na mapambano dhidi ya kuenea kwa virusi vya Covid-19 katika huko Seoul, Machi 12, 2020. YONHAP / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hali hiyo inajiri wakati mlipuko mpya wa janga hilo umeonekana katika kituo cha kuwahudumia watu waliostaafu huko Daegu, mji wa Kusini mwa Korea Kusini, ulioathirika zaidi na virusi hivyo.

Katika taarifa yake ya kila siku, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (KCDC) kimeripoti kesi mpya 152 zilizothibitishwa, na kufikisha jumla ya maambukizo nchini kufikia 8,565.

Chini ya visa 100 vya maambukizi viliripotiwa katika siku nne zilizopita.

Kati ya kesi hizo mpya, 97 zimeripotiwa huko Seoul, ikiwa ni pamoja na wagonjwa 74 katika kituo cha kuwahudumia watu waliostaafu ambao walipimwa wiki hii, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (KCDC) kimesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.