Pata taarifa kuu
DRC-SURUA-AFYA

DRC yaendelea kukumbwa na ugonjwa wa Surua

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaendelea kukabiliwa na janga kubwa la ugonjwa wa ukambi (au Surua). Katika mikoa mbalimbali, wazazi wamenyooshewa kidole cha lawama kwa kutowaharakisha wagonjwa hospitalini wanapoona dalili za ugonjwa huo zinaanza kujitokeza.

Ugonjwa wa Ukambi (au Surua) unaathiri mikoa karibu yote ya DRC
Ugonjwa wa Ukambi (au Surua) unaathiri mikoa karibu yote ya DRC © AFP PHOTO / LIONEL HEALING
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya vifo 4000 vimeipotiwa, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, watoto 200,000 wameambukizwa virusi vya ugonjwa huo hatari, ikiwa ni mara tatu zaidi ya mwaka jana. Ugonjwa hatari wa Ukambi umeathiri mikoa 26 ya nchi hiyo. Waathiriwa wengi ni watoto walio na umri wa miaka 5.

Kwa mujibu wa UNICEF, mwaka jana, asilimia 57 ya watoto walipata chanjo dhidi ya ugonjwa wa Ukambi wakati Shirika la Afya duniani, WHO, inapendekeza asilimia 95 ya chanjo kuzuia magonjwa ya milipuko. UNICEF imeatoa wito kwa Jumuiya ya kimataifa kuwekeza katika mpango wa kitaifa wa chanjo.

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, Ukambi (au surua) ni ugonjwa wa kuambukiza unaoenezwa sana kupitia mgusano yanayosababishwa na virusi vya ukambi.

Ishara na dalili za kwanza kwa kawaida hujumuisha homa, ambayo mara nyingi huwa zaidi ya 40 °C (104.0 °F), kikohozi, mafua, na macho mekundu. Siku mbili au tatu baada ya dalili kuanza, madoa madogo meupe yanaweza kuonekana ndani ya kinywa yanayojulikana kama alama za koplik. Chunusi nyekundu, zinazoanza kwenye uso kisha kuenea kwa mwili wote, kwa kawaida huanza siku tatu hadi tano baada ya mwanzo wa dalili, wameongeza wataalamu wa afya.

Dalili kwa kawaida huwa siku 10–12 baada ya kutangamana na mtu aliyeambukizwa kwa siku 7–10.

Matatizo zaidi ya ukambi hutokea kwa takriban asilimia 30 na yanaweza kujumuisha kuhara, upofu, inflamesheni ya ubongo, na nimonia miongoni mwa mengine, wamebaini wataalam wa afya.

Rubela na Roseola ni magonjwa tofauti ingawa yanafanana na Surua.

Ukambi ni ugonjwa unaoambukiza kupitia hewa na kuenezwa kwa urahisi na watu walioambukizwa kupitia kikohozi na kupiga chafya. Pia unaweza kuenezwa kupitia kutangamana na mate au makamasi. atu tisa kati ya kumi wasio na kingamwili wanaokaa pamoja na mtu aliyeambukizwa wataambukizwa ukambi. Watu huweza kuwaambukiza wengine katika siku nne kabla hadi siku nne baada ya mwanzo wa chunusi.

Watu kwa kawaida hupata ugonjwa huu mara moja tu. Vipimo vya virusi hivi katika visa vinavyokisiwa ni muhimu kama sehemu ya juhudi za afya ya umma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.