Pata taarifa kuu
DRC-AFYA-EBOLA

Mtu wa 1,000 aliye ambukizwa virusi vya Ebola apona Mashariki ma DRC

Maafisa wa afya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanasema mgonjwa wa 1,000 aliyepewa matibabu, baada ya kuambukizwa ugonjwa hatari wa Ebola, amepona na kurejea nyumbani.

Zoezi la chanjo ya Ebola lafanyika Goma Agosti 7, 2019.
Zoezi la chanjo ya Ebola lafanyika Goma Agosti 7, 2019. Augustin WAMENYA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hii ni dalili nzuri katika vita dhidi ya ugojwa huu ambao umesababisha vifo vya watu zaidi ya 2,000 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa muda wa mwaka mmoja uliopita, kwa mujibu wa maafisa wa afya.

Hata hviyo, kumekuwa na wasiwasi na mashaka iwapo chanjo au matibabu yanayotolewa yanasaidia kupambana na ugonjwa huu ambao umekuwa tishio katika eneo lote la Afrika Mashariki na Kati.

Pamoja na hilo, watalaam wa afya nchini humo wanasema bado wanakabiliwa na kaz kubwa ya kuwaomba wagonjwa kujitokeza na kukubali kupata matibabu.

Hata hivyo David Gressly, mwakilishi wa Umoja wa Mataifa anayeongoza mapambano dhidi ya Ebola nchini humo anasema kuwa taarifa za kupona kwa watu, zinawapa moyo wa kuendelea na vita dhidi ya ugonjwa huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.