Pata taarifa kuu

Ujumbe wa Marekani unatarajiwa nchini Niger wiki ijayo

Ujumbe wa Marekani unatarajiwa wiki ijayo mjini Niamey kujadiliana na serikali ya kijeshi ambayo hivi karibuni ilishutumu makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi, televisheni ya umma ya Nigerien imetangaza siku ya Ijumaa.

[Picha ya zamani] Katika picha hii iliyopigwa Aprili 16, 2018, bendera za Marekani na Niger zinapandishwa bega kwa bega katika kambi ya wanajeshi wa anga huko Agadez.
[Picha ya zamani] Katika picha hii iliyopigwa Aprili 16, 2018, bendera za Marekani na Niger zinapandishwa bega kwa bega katika kambi ya wanajeshi wa anga huko Agadez. AP - Carley Petesch
Matangazo ya kibiashara

 

"Ujumbe wa ngazi ya juu wa Marekani utakwenda Niamey wiki ijayo kutathmini ushirikiano wetu na kutoa mapendekezo madhubuti kwa upande wa Niger ili kufikiria vyema siku zijazo," imesema televisheni hiyo katika ripoti ya ziara ya Waziri Mkuu Ali Mahamane Lamine Zeine mjini Washington.

Katika mji mkuu wa Marekani ambako aliwasili siku ya Jumanne, Bw. Lamine Zeine alikutana na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje. "Kuimarishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi, kibiashara na kiteknolojia" kulijadiliwa haswa, kulingana na televisheni ya serikali ya Nigeria. Marekani ilisitisha ushirikiano wake muhimu, ukiwemo ushirikiano wa kijeshi na Niger baada ya mapinduzi yaliyompindua rais mteule Mohamed Bazoum Julai 26.

Kuhusu "ushirikiano wa kijeshi, Waziri Mkuu, kwa lugha ya wazi na bila miiko, alisisitiza uamuzi huru wa Niger wa kuomba kuondoka kwa majeshi yote ya kigeni, ikiwa ni pamoja na ya Marekani", inabainisha televisheni ya umma. Mwezi Machi, Niger ilishutumu makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi yaliyotiwa saini mwaka 2012 na Marekani, ikibaini kwamba "yaliwekwa kwa upande mmoja" na Washington.

Wanajeshi 1,000 wa Marekani waliopo Niger wanashiriki katika mapambano dhidi ya wanajihadi katika Sahel na wana kituo kikubwa cha ndege zisizo na rubani huko Agadez (kaskazini). Maelfu ya watu waliandamana mjini Niamey siku ya Jumamosi kuwataka waondoke bila kuchelewa.

Baada ya kuingia madarakani, utawala wa kijeshi uliitaka Ufaransa kuondoa wanajeshi wake kwenyz ardhi yake, jambo lilitekelezwa na Paris. Tangu wakati huo imeimarisha ushirikiano wake, hasa na Urusi ambayo ilituma karibu wakufunzi mia moja nchini Niger. Mjini Washington, Bw. Lamine Zeine pia alikutana na maafisa kutoka Benki ya Dunia (WB) kwa nia ya kurejesha malipo yake yaliyokatizwa baada ya mapinduzi.

Ufadhili wa WB nchini Niger, unaoundwa “hasa na misaada”, unakadiriwa kuwa zaidi ya dola bilioni 4 kwa nyanja ya elimu, afya, maendeleo ya vijijini, miundombinu na nishati. Ujumbe wa WB utakwenda Niger kukamilisha majadiliano na mamlaka, amesema Waziri Mkuu wa Niger.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.