Niger : Raia wameandamana kushinikiza kuondoka wa wanajehsi wa Marekani
Nchini Niger, kumekuwa na maandamano ya raia wa jimbo la Agadez kushinikiza kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani katika eneo lao.
Imechapishwa:
Cheza - 00:51
Hatua hii inakuja baada ya serikali ya Marekani siku ya Ijumaa kukubali kuondoa wanajeshi wake zaidi ya Elfu Moja, katika nchi hiyo, inayoongozwa na wanajeshi kwa sasa.
Hii ilitanguliwa na uongozi wa Niger, kutangaza kusitisha mara moja, ushirikiano wa kijeshi na Marekani, hatua ambayo pia imeungwa mkono na mashirika ya kiraia nchini humo.
Soma piaMarekani yakubali kuondoa kikosi chake cha kupambana na wajihadi Niger
Tangazo la Marekani kukubali kuondoa vikosi vyake ambavyo vimekuwepo nchini humo tangu mwaka 2013, kusaidia kupambana na makundi yenye silaha, inaonekana kama ushindi kwa Agadez êneo ambalo limekuwa ngome ya wanajeshi háo, ambao kwa wiki kadhaa sasa wamekuwa wakipata shinikizo ya kuondoka.
Wachambuzi wa mambo wanasema, hatua hiyo ya Marekani huenda ikaifaa Urusi ambayo imekuwa ikituma kikosi chake cha Wagner katika ukanda huo, katika nchi za Mali na Burkina Faso ambazo pia zinaongozwa na jeshi.
Douglas Omariba- RFI-Kiswahili Nairobi.