Pata taarifa kuu

Nigeria: MSF yaonya kuhusu kiwango kikubwa cha utapiamlo

Nairobi – Shirika la Kimataifa la Madaktari wasio na mipaka MSF linaonya kuhusu kiwango kikubwa cha utapiamlo na ukosefu wa mahitaji muhimu ya kibinadamu Kaskazini Magharibi mwa Nigeria.

Shirika la Kimataifa la Madaktari wasio na mipaka MSF
Shirika la Kimataifa la Madaktari wasio na mipaka MSF © Julie Remy/msf.fr
Matangazo ya kibiashara

MSF inasema hali hii imechangiwa na utovu wa usalama Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo ambapo, watu wenye silaha wameendelea kuwavamia watu, kuwauwa na kuwateka.

Mpaka sasa, Shirika hilo linasema limewatibu zaidi ya watoto Laki Moja na Elfu Sabini, wanaosumbuliwa na utapiamlo na wengine zaidi ya Elfu 32 wamelazwa hospitalini, wakiwa na hali mbaya.

Utovu wa usalama unasababisha wakaazi wa Kaskazini mwa Nigeria, kuishi maisha magumu kwa sababu hawawezi kujihusisha na shughuli za kiuchumi na sasa MSF inataka Umoja wa Mataifa na watoa misaada wa kimataifa kutambua hali hiyo na kuchukua hatua haraka.

Tangu mwaka 2009 mashirika mbalimbali yamekuwa yakijitokeza kuwasaidia watu zaidi ya Milioni 2 waliokimbia makaazi yao, lakini kuna uhaba mkubwa wa mahitaji ya kibinadamu hasa chakula, dawa, maji safi na makaazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.