Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Guinea-Bissau: Mawaziri wawili wa zamani washtakiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma

Nchini Guinea-Bissau, kesi ya maafisa wawili wa zamani wa serikali, mtawalia wanaohusika na fedha za umma na Hazina, ilianza Jumatatu Machi 11. Wanatuhumiwa kuchukua zaidi ya euro milioni tisa kutoka kwa hazina ya serikali, bila utaratibu wowote. Lakini baada ya kuanza kwa shida, ilibidi kesi hiyo iahirishwe kwa sababu kesi ilikuwa ya mvutano.

Moja ya maeneo ya mji mkuu wa Guinea-Bissau, Bissau,. (Picha ya kielelezo).
Moja ya maeneo ya mji mkuu wa Guinea-Bissau, Bissau,. (Picha ya kielelezo). © Charlotte Idrac / RFI
Matangazo ya kibiashara

Katika ufunguzi wa kusikilizwa kwa kesi hii katika Mahakama ya Rufaa ya Bissau, siku ya Jumatatu Machi 11, mawakili wa Souleiman Seidi na Antonio Monteiro, mtawalia aliyekuwa Waziri wa Uchumi na Fedha; na kaibu kiongozi kwenye wizara ya Fedha, waliona kuwa utaratibu huo ulikuwa kinyume na katiba.

Kwa sababu ni Ofisi ya Mapambano dhidi ya Ufisadi na Uhalifu wa Kiuchumi ndiyo iliyofanya uchunguzi na kusikilizwa kwa washtakiwa hao wawili. Hata hivyo, mawakili wao wanaamini kuwa Ofisi hii si halali katika kesi hii kwa vile iliundwa kufuatia agizo la Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na si kwa sheria baada ya kupigiwa kura Bungeni.

Upande wa utetezi pia unaitilia shaka mahakama yenyewe, ikidai kuwa haina mamlaka ya kuwafungulia mashitaka wawili hao waliokuwa maafisa wa serikali. Mijadala hiyo ilidumu kwa saa kadhaa, katika hali ya msukosuko mkubwa, hali iliyoiifanya mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi tarehe ambayo - kwa sasa - bado haijatangazwa.

Mapigano mwishoni mwa mwaka jana

Kama ukumbusho, waziri huyo wa zamani na katibu kiongozi kwenye Wizatra ya Fedha walikamatwa mwishoni mwa mwezi wa Novemba mwaka jana, baada ya kuchukua zaidi ya euro milioni tisa kutoka kwa hazina ya umma, "kusaidia wadau wa uchumi", walijitetea.

Usiku wa Novemba 30 kuamkia Desemba 1, baada ya kukamatwa kwao, askari wa kikosi cha walinzi wa taifa walijaribu kuwaachilia kwa nguvu. Mapigano kati ya jeshi na kikosi maalum cha walinzi wa taifa yalisababisha vifo vya watu wawili, kabla ya wahusika waliotaka kuwatorosha washtakiwa, kuweka chini silaha zao. Rais Umaro Sissoco Embalo alitaja matukio haya kama "jaribio la mapinduzi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.