Pata taarifa kuu
HAKI-SIASA

Viongozi wa ngazi za juu kukabiliwa na kesi ya jaribio la mapinduzi nchini Guinea-Bissau

Viongozi wakuu wa kisiasa na kijeshi nchini Guinea-Bissau, wakiwemo baadhi ya wapinzani wakuu wa Rais Umaro Sissoco Embalo, watakabiliwa na kesi kwa madai ya kuhusika katika kile kilichowasilishwa kama jaribio la mapinduzi mnamo Februari 1, 2022.

Le président bissau-guinéen, Umaro Sissoco Embalo, ici lors d'une conférence de presse en Afrique du Sud en avril 2022, a annoncé la dissolution du Parlement, ce lundi 4 décembre.
Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo, hapa wakati wa mkutano na waandishi wa habari nchini Afrika Kusini mwezi Aprili 2022, alitangaza kuvunjwa kwa Bunge Jumatatu hii, Desemba 4. © PHILL MAGAKOE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika orodha ya watu 20 walioitwa kujibu mashtaka ni mawaziri wakuu wa zamani Domingos Simoes Pereira na Nuno Gomes Nabiam, wakuu wa zamani wa majeshi Antonio Indjai na José Zamora Induta na wabunge kadhaa.

Mkuu wa zamani wa Jeshi la Wanamaji Jose Americo Bubu Na Tchuto, aliye juu ya orodha hiyo, amewasilishwa kama "kiongozi anayedaiwa wa jaribio la mapinduzi" katika waraka huu kutoka "tume huru ya uchunguzi" iliyoundwa baada ya matukio ya Februari 2022.

“Baada ya uchunguzi unaoendelea kuhusu shambulio dhidi ya ikulu ya rais na makao makuu ya serikali kwa kutumia silaha za kivita, watu waliotajwa hapo juu watafikishwa mahakamani kujibu makosa yanayodaiwa kufanywa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Guinea-Bissau na kwa kuzingatia kanuni ya kudhaniwa kuwa hawana hatia,” unasema waraka huu uambo shirika la habari la  AFP lilipata kopi siku ya Ijumaa. Hakuna tarehe iliyotajwa.

"Yeyote atakayepatikana na hatia atalipa kwa vitendo vyake. Watu hawawezi kukosa kuadhibiwa," Rais Embalo alisema siku ya Alhamisi, akizungumzia kesi hii miongoni mwa nyingine.

Watu wenye silaha walishambulia Ikulu ya rais na makao makuu ya serikali katika mji mkuu Bissau miaka miwili iliyopita wakati Rais Embalo alipokuwa akiongoza kikao cha baraza la mawaziri. Bw. Embalo alitokz bila kujeruhiwa baada ya saa kadhaa za kurushiana risasi na kusababisha vifo vya watu 11 kulingana na serikali.

Rais Embalo alielezea mapinduzi hayo kama yanayohusiana moja kwa moja na vita ambavyo anasema anaendesha dhidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya na ufisadi. Guinea-Bissau, nchi ndogo na maskini yenye takriban watu milioni mbili katika Afrika Magharibi, inachukuliwa kuwa kitovu cha biashara ya kokeini kutoka Amerika Kusini. Katika nchi ambapo nyadhifa za malipo ni adimu na zinazoshindaniwa, wanachama wengi wa vikosi vya jeshi waliopo kila mahali wanaaminika kuhusika katika usafirishaji haramu wa binadamu.

Tangu uhuru wake kutoka kwa Ureno mwaka 1974, Guinea-Bissau imekumbwa na msururu wa mapinduzi ya kijeshi au la, ambayo mara ya mwisho yalifanikiwa mwaka 2012. Tangu 2014, imejitolea kurejesha utaratibu wa kikatiba, ambao ulivurugika kutokana na misukosuko na hali ya mzozo wa kisiasa. Nchi hi pia ilikumbwa na tukio mnamo mwezi wa Desemba 2023 la mapigano kati ya jeshi na maafisa wa usalama ambayo yalisababisha vifo vya watu wawili na ambayo mkuu wa nchi pia alielezea kama jaribio la mapinduzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.