Pata taarifa kuu

Guinea-Bissau: Waziri Mkuu afutwa kazi siku nane baada ya kuteuliwa tena

Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo Jumatano alimfukuza kazi Waziri Mkuu ambaye alikuwa amemteua tena siku nane zilizopita baada ya kuvunjwa kwa Bunge la Kitaifa na makabiliano ambayo aliyataja kama "jaribio la mapinduzi ya serikali", kulingana na agizo la rais.

Geraldo João Martins ni kiongozi wa upinzani ambaye alishinda uchaguzi wa wabunge wa mwezi wa Juni karibu na chama cha kihistoria cha PAIGC.
Geraldo João Martins ni kiongozi wa upinzani ambaye alishinda uchaguzi wa wabunge wa mwezi wa Juni karibu na chama cha kihistoria cha PAIGC. © Aliu Candé
Matangazo ya kibiashara

"Bwana Geraldo João Martins anafukuzwa kutoka wadhifa wake kama Waziri Mkuu. Agizo hili linaanza kutumika mara moja," inaonyesha nakala iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP, bila kutoa maelezo zaidi.

Bw. Martins ni kiongozi wa muungano wa upinzani ambao ulishinda uchaguzi wa wabunge wa mwezi Juni karibu na chama cha kihistoria cha PAIGC, ambacho kiliongoza mapambano ya ukombozi wa Guinea-Bissau na kwa muda mrefu kimetawala maisha ya kisiasa ya nchi hii inayokabiliwa na ukosefu wa utulivu wa kudumu.

Aliteuliwa tena kama mkuu wa serikali mnamo Desemba 12 licha ya kuvunjwa kwa Bunge na Rais Embalo kutokana na makabiliano kati ya kikosi cha walinzi wa taifa na jeshi mnamo Desemba 1, na kusababisha vifo vya watu wawili katika mji mkuu Bissau.

Rais wa Guinea-Bissau alielezea matukio haya kama "jaribio la mapinduzi" wakati spika wa Bunge na mpinzani wa muda mrefu wa Bw. Embalo, alishutumu "mapinduzi ya kikatiba" akimhusisha Rais Embalo.

Mapigano hayo ya Desemba 1 yalianza wakati askari wa Jeshi la Ulinzi la Taifa walipoingia katika majengo ya polisi wa uchunguzi kuwachukua Waziri wa Uchumi na Fedha na katibu mkuu kiongozi katika Hazina ya Umma ambao walikuwa wakihojiwa kuhusiana na kutolewa kwa dola milioni kumi kutoka kwa hazina ya serikali.

Makabiliano haya yanaonekana kama kielelezo kipya cha migawanyiko ya kisiasa katikati mwa serikali, hali ambayo pia huvikumba vikosi vya usalama. Tangu uhuru wake kutoka kwa Ureno mwaka 1974, Guinea-Bissau imekumbwa na msururu wa mapinduzi au majaribio ya mapinduzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.