Pata taarifa kuu

Katika mstari wa mbele, vijana wa Burkina Faso wanajipanga kupinga ukeketaji

Burkina Faso, mojawapo ya nchi zilizoathiriwa zaidi na ukeketaji, inafanya maendeleo ya kutia moyo katika mapambano dhidi ya tabia hii mbaya. Uhamasishaji wa vijana, wasichana na wavulana, ni kipengele muhimu katika mienendo hii chanya.

Amran Mahamood, ambaye amejikimu kimaisha kwa miaka 15 kwa kuwafanyia ukeketaji wasichana wadogo, anakaa karibu na msichana mnamo Februari 19, 2014 huko Hargeysa.
Amran Mahamood, ambaye amejikimu kimaisha kwa miaka 15 kwa kuwafanyia ukeketaji wasichana wadogo, anakaa karibu na msichana mnamo Februari 19, 2014 huko Hargeysa. © Nichole Sobecki /AFP
Matangazo ya kibiashara

Ukeketaji unazidi kupungua nchini Burkina Faso, matokeo mazuri yamepatikana kutokana na kujitolea kwa Serikali kwa miaka kadhaa, lakini pia kwa vijana, wasichana na wavulana, ambao wanahamasisha dhidi ya "uovu huu mkubwa".

Vurugu za makundi ya kijihadi na madhara yake kwa raia, hata hivyo, yanatishia mwelekeo wa kushuka katika nchi hii ya Sahel yenye wakazi milioni 23, wengi wao wakiwa wanawake. Ni mojawapo ya nchi 29 zilizoathiriwa zaidi na ukeketaji duniani, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, lakini maendeleo makubwa yamerekodiwa nchini humo kwa zaidi ya miaka 10.

Mnamo 2010, 76% ya wasichana na wanawake wa umri wa miaka 15 hadi 49 walikuwa waathiriwa: miaka kumi na moja baadaye, mnamo 2021, walikuwa 56% tu. Kupungua ambako, kwa kiasi kidogo, pia kunahusu visa vya ukeketaji wa watoto wenye umri wa miaka 0 hadi 14, kushuka kutoka 13% mwaka 2010 hadi 9% mwaka 2021.

Bilal Sougou, mkuu wa mpango wa ulinzi wa watoto katika Unicef-Burkina, anakaribisha "maendeleo haya muhimu" yanayohusishwa na "dhamira kubwa ya kisiasa kutoka kwa mamlaka". 

Lakini, anabainisha Roukiatou Sedgo, mratibu wa mradi wa "Living with Excision" ambao unaorodhesha wanawake waliofanyiwa ukeketaji, "bado tuna matatizo katika mikoa ya Kaskazini, Sahel na Kusini-Magharibi", miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi na ghasia za wanajihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.