Pata taarifa kuu

Idadi ya waathirika wa vitendo vya ukeketaji kidunia imefikia watu milioni 230

Nairobi – Ripoti mpya ya shirika linalohudumia watoto, UNICEF, inaonesha kuwa idadi ya waathirika wa vitendo vya ukeketaji kidunia imefikia watu milioni 230, ikiwa ni ongezeko la asilimia 15 tangu mwaka 2015 licha ya hatua kupigwa kwenye mataifa ambayo jamii zimekuwa zikitekeleza vitendo hivi.

Ripoti mpya ya shirika linalohudumia watoto, UNICEF, inaonesha kuwa idadi ya waathirika wa vitendo vya ukeketaji kidunia imefikia watu milioni 230
Ripoti mpya ya shirika linalohudumia watoto, UNICEF, inaonesha kuwa idadi ya waathirika wa vitendo vya ukeketaji kidunia imefikia watu milioni 230 © REUTERS/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa muandishi kinara wa ripoti hiyo, Claudia Coppa, “habari hii sio nzuri kutokana na idadi kuwa kubwa zaidi kuwahi kuripotiwa, ripoti iliyotolewa sambamba na siku ya kimataifa ya wanawake.

Bara la Afrika linatajwa kuongoza kuwa na idadi kubwa zaidi ya wathiriwa wa ukeketaji ikiwa na zaidi ya watu milioni 144, ikifuatiwa na Asia (milioni 80) na Mashariki ya Kati (milioni sita), kulingana na utafiti wa nchi 31 ambapo mila hiyo ni ya kawaida.

Hata hivyo licha ya ripoti kuonesha kuna ongezeko, baadhi ya nchi zimeripoti kupungua kwa vitendo vya ukeketaji, ikiwemo Sierra Leone, Ethiopia, Burkina Fasi na Kenya.

Tendo la ukeketaji dhidi ya wasichana, linahusisha kukata kisimi na eneo la Labia, na huweza kusababisha mtu kutokwa na damu, kupata maambukizo au pia kuwa na madhara ya muda mrefu kama vile matatizo ya uzazi, shida wakati wa kujifungua au maumivu wakati wat endo la ndoa.

Wanaharakati sasa wanayataka mataifa kuongeza kasi hasa katika kudhibiti vitendo hivi kwa kuelimisha jamii na kutunga sharia kali dhidi ya wanaotekeleza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.