Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Burkina Faso: Mahakama yaagiza kuachiliwa kwa wakili Guy-Hervé Kam

Nchini Burkina Faso, Mahakama imeagiza, Alhamisi hii, Machi 7, kuachiliwa mara moja kwa wakili Guy-Hervé Kam. Alikamatwa na wanaume waliovalia kiraia mnamo Januari 24 katika uwanja wa ndege wa alitangaza kwamba wakili na pia mwanasiasa anashitakiwa "kuhatarisha usalama wa taifa" kwa kujaribu kuhamasisha wanafunzi na viongozi wa kijadi.

Siku ya Alhamisi Machi 7, mahakama imeagiza kuachiliwa mara moja kwa wakili Guy-Hervé Kam, wakili na pia mwanaharakati wa haki za binadamu.
Siku ya Alhamisi Machi 7, mahakama imeagiza kuachiliwa mara moja kwa wakili Guy-Hervé Kam, wakili na pia mwanaharakati wa haki za binadamu. DR
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na mwanasheria wake, kukamatwa kwa wakili  Guy-Hervé Kam hakujazingatia utaratibu wowote. Na kulingana na jaji wa mahakama ya utawala, kuzuiliwa kwake kunakiuka uhuru wa kimsingi wa wakili. Tangu Januari 24, mwanzilishi mwenza wa vgvugu la Balai Citoyen anazuiliwa bila mawakili wake kuweza kumtembelea.

Wanasema wameridhika na uamuzi huu, unaochochewa na "sheria", kulingana na wakili Prosper Farama. "Kinachoombwa kwa Guy-Hervé Kam sio kutokujali bali kuheshimu haki zake," amesema.

Utetezi wa Guy-Hervé Kam unasisitiza kwamba ikiwa serikali ya Burkina Faso ina jambo la kumsuta mteja wake, "mashtaka haya lazima yatekelezwe kwa utaratibu wa kawaida, ambao unaheshimu viwango vilivyotolewa na nakala yetu".

Maamuzi ya mahakama hayatekelezwi kila wakati

Haijulikani ikiwa serikali inakusudia kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu, au kufuata uamuzi huo na kumwachilia kiongozi wa vuguvugu la kisiasa la Sens.

Uzoefu wa hivi majuzi unaonyesha kuwa nchini Burkina Faso, maamuzi ya mahakama hayatumiki kila mara. Mwezi Novemba mwaka jana, mahakama hiyo iliagiza kuachiliwa kwa mfanyabiashara Anselme Kambou, bila mafanikio.

Mnamo mwezi Desemba, mahakama hiyo ilibatilisha maombi ya kijeshi dhidi ya Rasmané Zinaba na Bassirou Badjjo wa vuguvugu la Balais Citoyen, ambayo hayakuzuia watu hawa wawili kukamatwa Februari iliyopita, kulingana na utaratibu wa kawaida wa uendeshaji, ambao unakumbusha jinsi baadhi ya raia wa Burkina Faso wanalazimishwa kuandikishwa katika jeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.