Pata taarifa kuu

Guinea-Bissau imesitisha malipo ya walimu ilikuondoa wafanyikazi gushi

Nairobi – Serikali ya Guinea-Bissau, imeagiza kusimamishwa kwa mishahara ya walimu ili kuondoa madai ya udanganyifu kwenye orodha ya mishahara kutoka kwa wafanyikazi gushi.

Rais wa  Guinée-Bissau, Umaro Sissoco Embaló.
Rais wa Guinée-Bissau, Umaro Sissoco Embaló. © AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Taifa hilo la Afŕika Maghaŕibi ambalo linategemea kwa kiasi kikubwa misaada ya nje kukidhi mishahara katika sekta ya elimu, limetangaza vita dhidi ya watumishi wa umma hewa ili kupunguza sehemu kubwa ya fedha zinazoelekezwa kwenye mishahara.

Uamuzi wa Julai 18 wa baraza la mawaziri wa nchi hiyo siku ya Alhamis uliagiza wizara ya elimu kufanya sensa ya idadi ya wafanyikazi wake.

Hatuo hiyo itaathiri walimu 8,000 katika shule za msingi na sekondari nchini humo ambao wanapata wastani wa faranga za CFA 50,000 ($86) kwa mwezi.

Domingos de Carvalho, rais wa muungano wa kitaifa wa walimu wa Bissau, alisema chama hicho kitakata rufaa dhidi ya uamuzi huo ambao umesema sio wa haki.

"Hatupangii hatua yoyote ya mgomo, lakini tunafikiria kutafuta njia zingine mwafaka za kujibu," de Carvalho alisema.

Nchi hiyo ina idadi ya watu milioni 2.1,  kiwango asilimia 56 ya raia wake wakiwa na uwezo wa kusoma na kuandika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.