Pata taarifa kuu

Nchi za Niger, Mali na Burkina Faso zatangaza kuunda jeshi la pamoja

Nairobi – Niger, Mali na Burkina Faso zimetangaza kuunda jeshi la pamoja, kupambana na makundi ya kijihadi katika nchi zao.

Hata hivyo,mamlaka haijaeleza kikosi cha jeshi hilo linaundwa na wanajeshi wangapi
Hata hivyo,mamlaka haijaeleza kikosi cha jeshi hilo linaundwa na wanajeshi wangapi © RFI
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Majeshi wa Niger, Moussa Salaou Barmou ametangaza muungano huo, akisema operesheni ya jeshi hilo la pamoja, itaanza hivi karibuni.Hata hivyo, hajaeleza kikosi cha jeshi hilo linaundwa na wanajeshi wangapi.

Hatua hii inakuja baada ya mwezi Septemba mwaka uliopita, nchi hizo ambazo pia zilitangaza kujiondoa kwenye Jumuiya ya ECOWAS, zilitangaza muungano mpya wa kijeshi baada ya kujiondoa kwenye kikosi cha kimataifa cha G5.

Hali ya usalama katika nchi hizo tatu, imeendelea kuwa mbaya kwa muda wa miaka 10 kutokana na uwepo wa makundi ya kijihadi na kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa, koloni ya zamani ya nchi hizo tatu, imesababisha hali kuendelea kuwa mbaya.

Jeshi hilo la pamoja, pia linatarajiwa kuchukua nafasi ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa MINUSMA, ambacho mwezi Desemba mwaka uliopita, liliondoka kwenye nchi hizo baada ya kufukuzwa na viongozi wa kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.