Pata taarifa kuu

Burkina: Mauaji ya raia Februari 25 yalisababisha vifo vya watu 170 kaskazini-magharibi

Nchini Burkina Faso, mauaji ya raia yanaendelea... Taarifa imetolewa kuhusu vifo vya angalau watu 170 katika wilaya tofauti za mkoa wa Yatenga, kaskazini-magharibi mwa nchi. Mauaji hayo yanatisha, yaliyomfanya mwendesha mashtaka wa nchi kuguswa katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Maafisa wa jeshi la Burkinabe wakishika doria huko Kaya, mji mkuu wa mkoa wa kaskazini-kati wa Burkina Faso, Novemba 20, 2021 (Picha ya kielelezo).
Maafisa wa jeshi la Burkinabe wakishika doria huko Kaya, mji mkuu wa mkoa wa kaskazini-kati wa Burkina Faso, Novemba 20, 2021 (Picha ya kielelezo). AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

Kulingana kutoka kwa mwendesha mashtaka katika Mahakama Kuu ya Ouahigouya, matukio hayo yalifanyika Jumapili Februari 25 katika maeneo matatu katika jimbo la Thiou. Vijiji vinavyohusika, kulingana na Mwendesha Mashtaka, ni vile vya Komsilga, Nodin na Soro.

Kulingana na shuhuda zilizokusanywa na RFI Mandenkan, wahanga ni wanaume, wanawake lakini pia watoto wadogo. Wangekuwa - kulingana na tukio la bahati mbaya linalojirudia -ni wahanga wa mashambulio ya magaidi na majibu ya vikosi vya serikali.

Katika kesi hiyo, chanzo chetu cha habari kinatufafanulia kuwa kambi mbili za Wanajitolea kwa ajili ya Ulinzi wa Nchi (VDP) zilizoko nje kidogo ya eneo la Ouahigouya zilishambuliwa na wanajihadi siku ya Jumapili Februari 25, karibu saa moja asubuhi (saa za huko). Karibu wpiganaji wa VDP kumi waliuawa katika shambulio la magaidi na, karibu saa nne mchana,  wakati wa majibu kutoka kwa Wanajeshi wa serikali, wanakijiji walikuwa waathirika, kwa upande wake, kitendo kilichotekelezwa na watu wenye silaha.

Wahusika wa mauaji hayo ni akina nani?

Haiwezekani kusema kwa uhakika ikiwa wahusika wa mauaji haya ni magaidi au vikosi vya serikali ambavyo vinaweza kuchukua hatua ya kulipiza kisasi. Hii bila shaka ndiyo sababu mwendesha mashtaka katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, anasema kuwa uchunguzi utaanzishwa ili kubaini wajibu wa kia pande na kubaini wahusika wa mauaji haya.

Kwa ukumbusho, tangazo kama hilo lilitolewa wakati wa mauaji ya Zaongo mnamo mwezi wa Novemba, ambayo yalisababisha vifo vya watu 70, na huko Karma - itakuwa mwaka mmoja uliopita mwezi Aprili - kulikotokea mauaji ambayo yalisababisha karibu vifo vya watu 200. Katika visa vyote viwili, matokeo ya uchunguzi rasmi bado hayajajulikana.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani inasema inasikitishwa sana na ongezeko la ghasia zinazofanywa dhidi ya raia na magaidi na vikosi vya jeshi na ulinzi vya Burkina Faso.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.