Pata taarifa kuu

Waziri Mkuu wa zamani wa Togo Agbéyomé Kodjo afariki akiwa uhamishoni

Mwanasiasa wa upinzani wa Togo na Waziri Mkuu wa zamani Agbéyomé Kodjo, ambaye alishika nafasi ya pili katika uchaguzi wa rais wa mwka 2020, alifariki Jumapili akiwa uhamishoni akiwa na umri wa miaka 69, mmoja wa viongozi wa muungano wa vyama vya siasa ameliambia shirika la habari la  AFP siku ya Jumatatu.

Agbeyomé Kodjo, aliyekuwa Waziri Mkuu wa hayati Rais wa Togo Gnassingbé Eyadema, na mgombea urais wa chama cha MPDD.
Agbeyomé Kodjo, aliyekuwa Waziri Mkuu wa hayati Rais wa Togo Gnassingbé Eyadema, na mgombea urais wa chama cha MPDD. AFP Photo: Emile KOUTON
Matangazo ya kibiashara

"Agbéyomé Kodjo alifariki siku ya Jumapili nchini Ghana, kufuatia kuugua," Thomas Kokou N'soukpoe, mmoja wa viongozi wa Dynamique Monseigneur Kpodzro (DMK), muungano wa vyama vya siasa uliomuunga mkono mwanasiasa huyo wa upinzani katika uchaguzi wa urais 2020, ameliambia shirika la habari la AFP.

Bw. Kodjo alipata 19.46% ya kura katika uchaguzi wa urais mnamo Februari 22, ikilinganishwa na 70.78% ya Faure Gnassingbé, kulingana na matokeo rasmi ambayo amekuwa akiyapinga kila wakati. Mnamo mwezi wa Julai 2020, mpinzani huyo alikimbilia Togo, kufuatia kuitishwa mahakama na waranti wa kimataifa wa kukamatwa dhidi yake.

Waziri Mkuu wa zamani mwanzoni mwa miaka ya 2000, Agbéyomé Kodjo alishikilia nyadhifa kadhaa za uwaziri chini ya Jenerali Gnassingbé Eyadéma ambaye alitawala Togo kwa mkono wa chuma kwa miaka 38.

Bw. Kodjo alifukuzwa kazi mwaka wa 2002 na kufungwa kwa miezi michache nchini Togo, kabla ya kujiunga na upinzani na kuunda mwaka 2008, chama chake cha OBUTS, ambacho mwaka 2018 likawa chama cha Wazalendo Demokrasia na Maendeleo (MPDD).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.