Pata taarifa kuu

Niger: Ujumbe wa Togo wazuru Niamey baada ya kutangaza kujiondoa ECOWAS

Je, hili linaweza kuwa jaribio la kwanza la upatanishi kufuatia tangazo la Niger kujiondoa katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS ? Siku ya Jumatatu, ujumbe ulioongozwa na Waziri wa Utawala wa Togo ulipokelewa na mamlaka ya mpito mjini Niamey. Haijabainishwa  kama mkutano huu uliofanyika kwa siri, ambapo maudhui ya majadiliano hayakuwekwa wazi, ni kwa mpango wa ECOWAS au wa nchi ya Togo pekee.

[Picha ya kielelezo] Moja ya mitaa ya Niamey mnamo Septemba 8, 2023.
[Picha ya kielelezo] Moja ya mitaa ya Niamey mnamo Septemba 8, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

 

Kanali Hodabalo Awaté, Waziri wa Utawala wa Togo, ndiye ambaye alipokelewa na Jenerali Salifou Mody, Waziri wa Ulinzi wa Niger. Ziara hii, ambayo haikutangazwa hadharani, ilitangazwa kwa mara ya kwanza kwenye ukurasa wa Facebook wa wizara ya Niger, ikionyesha picha ya mkutano kati ya maafisa hao wawili wakuu.

"Ziara hii ya kikazi", ambayo inakuja siku moja baada ya Niger na majirane zake, Burkina Faso na Mali kutangaza kujiondoa katika ECOWAS, inaonyesha uhusiano mzuri ambao nchi hii inaimarisha na Togo.

Siku ya Alhamisi ya wili iliyopita, wakati wajumbe wa ECOWAS wakitarajiwa mjini Niamey, ni wanadiplomasia wa Togo pekee waliofanya ziara hiyo, wengine wakihalalisha kutokuwepo kwao kwa "matatizo ya kiufundi" ya ndege yao. "nia mbaya" ametangaza Waziri Mkuu wa Niger Lamine Zeine.

ECOWAS, ambayo Rais wa zamani Gnassingbé Eyadema, yeye mwenyewe ni kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi, ni mmoja wa waanzilishi, inasalia kuwa jumuiya muhimu ya kihistoria kwa Togo. Kulingana na mtafiti Niagalé Bagayoko, nchi hiyo imechukua nafasi ya mpatanishi kati ya ECOWAS na serikali za kijeshi tangu mapinduzi ya kijeshi nchini Mali mwaka 2020. Lakini kutokana na kuondoka kwa AES kutoka kwa kundi la Afrika Magharibi, waangalizi kadhaa wamebaini kushindwa kwa majadiliano haya.

Waziri wa Utawala wa Togo, Hodabalo Awaté, amehojiwa na RFI, lakini hakutaka kutoa maoni yake kuhusu mkutano wa Niamey.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.