Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-DEMOKRASIA

Uchaguzi wa wabunge na wa magavana kufanyika Aprili 13 nchini Togo

Uchaguzi wa wabunge na wa magavana utafanyika Aprili 13 nchini Togo, serikali ilitangaza siku ya Alhamisi jioni kwenye televisheni ya taifa. Uchaguzi huu wa wabunge utaambatana na uhaguzi wa magavana, ambao Togo itaandaa kwa mara ya kwanza.

Uchaguzi wa wabunge wa mwaka 2018 ulisusiwa na upinzani ambao ulishutumu "makosa" katika sensa ya wapiga kura.
Uchaguzi wa wabunge wa mwaka 2018 ulisusiwa na upinzani ambao ulishutumu "makosa" katika sensa ya wapiga kura. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Mnamo mwezi wa Novemba serikali ilitangaza kwamba uchaguzi huu utafanyika "mwisho wa robo ya kwanza ya mwaka 2024".

“Kwa mujibu wa masharti ya kanuni za uchaguzi na kwa kuzingatia ratiba iliyopendekezwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Baraza la Mawaziri lilipanga tarehe ya uchaguzi wa wabunge na wa magavana Jumamosi Aprili 13, 2024, na kuitisha, chombo cha maalumu kwa ajili ya uchaguzi huo,” almesema Yawa Kouigan, waziri wa mawasiliano na msemaji wa serikali.

Kiasi cha dhamana kimewekwa kuwa faranga za CFA 500,000 (sawa na euro 762.25) kwa kila mgombea wa uchaguzi wa wabunge, na faranga za CFA 200,000 (euro 304.90) kwa kila mgombea wa uchaguzi wa magavana, ameongeza. Kampeni ya uchaguzi itafanyika kuanzia Machi 28, 2024 saa 6:00 asubuhi hadi Aprili 11, 2024 saa 5:59 usiku.

Kama ilivyokuwa katika chaguzi zilizopita, "vikosi vya ulinzi, vikosi vya usalama, vikosi vya jeshi na akiba ya kazi" vitapiga kura mapema saa 72 kabla ya siku ya kupiga kura ya jumla, ili kuwawezesha kulinda usalama wa raia wakati wa kupiga kura.

"Ukiukwaji" katika sensa

Serikali pia imeheshimu mila kwa kuunda kitengo cha usalama, kilichoitwa "Kikosi cha Usalama cha Kisheria na Uchaguzi cha Mkoa 2024", "kwa nia ya kuhakikisha usalama wa nchi unazingatiwa" wakati na baada ya uchaguzi. Mnamo mwezi Januari, Bunge la taifa la Togo lilirekebisha sheria iliyoongeza idadi ya wabunge wa chaguzi hizi za wabunge kutoka 91 hadi 113.

Chaguzi za mwisho za wabunge zilifanyika mwaka wa 2018 na zilisusiwa na upinzani ambao ulishutumu "makosa" katika sensa ya uchaguzi. Wakati huu, upinzani unajiandaa kutoa changamoto kwa chama tawala, Union for the Republic (UNIR), na uliwahamasisha kwa nguvu wafuasi wake wakati wa sensa ya mwisho ya uchaguzi.

Rais Faure Gnassingbé aliingia madarakani mwaka wa 2005 baada ya kifo cha babake, Jenerali Gnassingbé Eyadéma, ambaye alitawala Togo kwa mkono wa chuma kwa miaka 38. Tangu wakati huo amechaguliwa tena mara tatu katika chaguzi ambazo zote zilipingwa na upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.