Pata taarifa kuu

Ghana: Sheria mpya dhidi ya watu wa LGBTQ yapitishwa na Bunge

Adhabu itakayotolewa ni kifungo cha hadi miaka mitatu jela kwa watu wanaotambuliwa kuwa ni kutoka jamii ya wapenzi wa jinsia moja (LGBTQ), hadi miaka mitano kwa yeyote anayeunga mkono jamii hii. Sheria ambayo inaweza tu kuanza kutumika kwa idhini ya rais. Nana Akuffo-Addo anatarajiwa kuzungumzia hatua hii chini ya wiki moja. Lakini mashirika mbalimali nchini Ghana na yale ya kimataifa yanashutumu sheria hii.

Wanaharakati wa LGBT+ waandamana kupinga mswada unaominya jamii yao, Oktoba 11, 2021.
Wanaharakati wa LGBT+ waandamana kupinga mswada unaominya jamii yao, Oktoba 11, 2021. AP - Emily Leshner
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Accra, Victor Cariou

Mashambulizi makubwa dhidi ya haki za kimsingi za watu, hatua zisizo za kikatiba... Ukosoaji wa mataifa ya kimataifa na yale ya nchini Ghana unaendelea dhidi ya muswada huu mpya wenye kichwa cha habari: "Haki za kijinsia za binadamu na maadili ya familia". Haijalishi kulingana na Sam George, anaye ungamkono muswada huo, uliopitishwa Jumatano Februari 28: kulingana na ySam George, ni juu ya kulinda watoto.

"Sheria hii inalenga kukomesha shambulio la baadhi ya watu kutoka Magharibi, ambao wanajaribu kubadilisha utamaduni wa Ghana. Kwa sababu ni lazima tulinde watoto na maambo yote yaliyo kinyume na utamaduni wetu,” amesema.

Katika kesi ya kile ambacho sheria inakiita "kukuza" kwa utamaduni wa LGBTQ, kifungo cha juu cha miaka mitano. Hatua isiyo na msingi na ya hatari, ambayo itaimarisha tu ubaguzi na hata vurugu kulingana na Michael Akagbro, wa shirika lisilo la kiserikali la Kituo cha Maendeleo ya Kidemokrasia cha Ghana: "Hata kabla ya kupitishwa kwa muswada huyu na Bunge, wanachama wa jamii ya LGBTQ walikuwa tayari wameshambuliwa katika tmaeneo tofauti ya nchi. Sheria hii itafanya hali kuwa mbaya zaidi. Kwa sababu kwa sheria hii, jamii itazingatia kuwa ina haki ya kuendeleza mashambulizi haya, kwa sababu itaungwa mkono na sheria hii. "

Michael Akagbro anabaini: shirika lake, kama mashirika meyingine nchini Ghana, litachukua hatua za kisheria ikiwa sheria hii itadhinishwa na rais chini ya wiki moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.