Pata taarifa kuu

Ghana: John Mahama apinga pendekezo kubadilishwa kwa tarehe ya uchaguzi

Nairobi – Mgombea wa urais kwa tiketi ya upinzani nchini Ghana John Mahama, amepinga mapendekezo ya kusongesha mbele tarehe ya uchaguzi mkuu kutoka mwezi Desemba mwaka huu hadi mwezi Novemba.

John Dramani Mahama- Mgombea wa urais nchini Ghana
John Dramani Mahama- Mgombea wa urais nchini Ghana © Reuters/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi kwenye taifa hilo (EC) mapendekezo hayo yalikuwa yametolewa na vyama vya kisiasa ilikutoa nafasi kwa tume hiyo kupata muda wa kutosha kujiandaa kuendesha shughuli zake na kujipanga iwapo kutahitajika duru ya pili ya uchaguzi.

Mahama ambaye ni mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha National Democratic Congress (NDC) amesema mabadiliko hayo ya tarehe ya uchaguzi hayawezekani.

Aidha kiongozi huyo wa upinzani ameeleza kuwa mabadiliko hayo hayajapendekezwa kwa faida ya raia akiituhumu tume ya uchaguzi kwa kukosa kujiandaa kusimamia uchaguzi huo.

John Mahama amepinga mapendekezo hayo ya tume ya uchaguzi
John Mahama amepinga mapendekezo hayo ya tume ya uchaguzi ittelecomdigest.com

Rais huyo wa zamani ametoa wito kwa tume ya uchaguzi kujiweka sawa ilikuhakikisha kuwa inasimamia uchaguzi huru na wa haki.

Kanisa na kiadiventisti nalo  pia lilikuwa limeiomba tume hiyo kubadilisha mbele siku ya uchaguzi kutoka siku ya kawaida ya Desemba 7 kwa sababu inaona na siku ya Jumamosi, siku yake ya ibada.

Haijabainika iwapo mapendekezo hayo mapya yanahusiana na ombi la  kanisa la kutaka kubadilishwa kwa siku ya uchaguzi.

Tume ya uchaguzi pia inawazia kutangaza siku ya kufanyika kwa zoezi hilo kuwa siku ya mapumziko ilikutoa nafasi kwa watu wengi kushiriki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.