Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Ghana: Makamu wa Rais Bawumia azindua kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa urais

Makamu wa Rais wa Ghana Mahamudu Bawumia, mgombea wa chama tawala katika uchaguzi wa rais wa mwezi Desemba, amezindua kampeni yake siku ya Jumatano mjini Accra kwa kupigia debe rekodi yake ya usimamizi wa uchumi na ajenda yake ya digitali.

Makamu wa Rais wa Ghana Mahamudu Bawumia, mgombea wa chama cha New Patriotic Party (NPP) katika uchaguzi wa urais wa mwezi wa Desemba, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni yake ya urais mjini Accra, Februari 7, 2024.
Makamu wa Rais wa Ghana Mahamudu Bawumia, mgombea wa chama cha New Patriotic Party (NPP) katika uchaguzi wa urais wa mwezi wa Desemba, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni yake ya urais mjini Accra, Februari 7, 2024. © Nipah Dennis / AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Uchaguzi wa urais nchini Ghana unaonekana kupambaniwa kati ya Bw. Bawumia, mgombea wa kwanza Muislamu wa chama cha New Patriotic Party (NPP), na rais wa zamani John Dramani Mahama, wa chama cha upinzani cha National Democratic Congress (NDC). Rais anayemaliza muda wake Nana Akufo-Addo anajiondoa kwenye kinyang'anyiro hiki baada ya mihula miwili huku uchumi wa nchi hiyo ukitoka katika moja ya matatizo yake mabaya zaidi kuwahi kutokea kwa miongo kadhaa.

"Licha ya uchumi mgumu tuliorithi, ilitubidi kujitokeza na kuanza kutatua matatizo," Bawumia amesema katika hotuba yake iliyopewa jina la "Ukurasa unaofuata nchini Ghana" katika hafla ya kongamano la hadhara lililoandaliwa katika mji mkuu wa Ghana kuwasilisha maono yake ya urais miezi kumi kabla ya uchaguzi.

Katika ukumbi wenye uwezo wa kupokea watu 5,000, na mbele ya mawaziri na maafisa wengi wa serikali, viongozi wa kidini na wanadiplomasia, Bw. Bawumia, naibu gavana wa zamani wa Benki Kuu, ametangaza kwamba ataifanya sekta binafsi kuwa injini ya ukuaji kwa utaratibu ili kutengeneza ajira zaidi kwa vijana na kuendeleza miundombinu.

Pia amesema atapunguza idadi ya mawaziri hadi kufikia 50 ili kupunguza matumizi. Alipoingia madarakani mwaka wa 2017, Akufo-Addo aliteua mawaziri 110. Mnamo 2022, Ghana ilipata mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi katika miongo kadhaa, na mfumuko wa bei wa zaidi ya 50%, na kulazimisha nchi hiyo ambayo ni mzalishaji mkuu wa dhahabu, mafuta na kakao kuchukua mkopo wa dola bilioni 3 kutoka kwa IMF na kufanya marekebisho ya deni lake. .

Deni la Ghana limeongezeka na, kama nchi nyingine za Kusini mwa Jangwa la Sahara, imelazimika kukabiliana na kuzorota kwa uchumi kutokana na janga la kimataifa la coronavirus na vita kati ya Urusi na Ukraine. Kupungua kwa mfumuko wa bei na utulivu wa sarafu ya nchi katika miezi ya hivi karibuni kunaonyesha kuimarika kwa hali ya uchumi wa nchi.

Bw Bawumia pia amesema atapanua wigo wa ushuru na kuongeza ukusanyaji wa mapato kupitia mfumo wa kidijitali, kipaumbele chake kingine. "Lengo langu ni kuondoa mgawanyiko wa kidijitali kwa kufikia kiwango cha intaneti cha kupenya karibu na 100%," amesema. Uchumi utakuwa mada kuu ya kampeni hiyo, huku upinzani ukitaka kuwasilisha mpango wa IMF kama ushahidi wa kushindwa kwa usimamizi wa uchumi wa NPP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.