Pata taarifa kuu

Ethiopia: Vikosi vya jeshi la serikali vyatuhumiwa mauaji ya 'raia 45' Merawi

Vikosi vya serikali ya Ethiopia viliwaua wakazi wasiopungua 45 wa mji moja katika jimbo la Amhara (kaskazini) mnamo Januari 29, ambapo walipambana na wanamgambo wa eneo hilo, Tume ya Haki za Kibinadamu ya Ethiopia (EHRC) imeshutumu leo Jumanne.

Wanajeshi kutoka Jeshi la Kitaifa la Ulinzi la Ethiopia wakati wa mafunzo huko Amhara mnamo Septemba 14, 2021.
Wanajeshi kutoka Jeshi la Kitaifa la Ulinzi la Ethiopia wakati wa mafunzo huko Amhara mnamo Septemba 14, 2021. © Amanuel Sileshi AFP/File
Matangazo ya kibiashara

 

Taasisi ya umma inayojitegemea kisheria, EHRC inazingatia katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba tathmini hii iko chini ya ukweli kwa sababu, kushindwa kuwa na uwezo wa "kukusanya taarifa kamili kutokana na hali ya usalama" hasa, "kazi yake ya uchunguzi haikuweza kufanyika kikamilifu.

EHRC inaeleza kuwa inachunguza "wahanga wa kiraia kufuatia mapigano kati ya vikosi vya usalama vya serikali na Fano", wanamgambo wa Amhara, mnamo Januari 29, 2024 huko Merawi, eneo la takriban kilomita 30 kusini mwa mji mkuu wa mkoa wa Bahir Dar. "Kulingana na uchunguzi wa kina, ukaguzi uliofanywa na EHRC ulifanya iwezekane kuthibitisha utambulisho wa angalau raia 45 waliouawa na vikosi vya usalama vya serikali, kwa sababu walituhumiwa kuunga mkono Fano," inabainisha taasisi hiyo.

Vurugu nyingi za kisiasa

EHRC pia inaeleza kwamba mnamo Januari 19, "angalau watu 15, wakiwemo wanawake (...) waliuawa" katika eneo la Yeidwuha (karibu kilomita 160 kusini mwa Bahir Dar), "wakati wa operesheni ya msako wa kimfumo wa nyumba zilizo karibu na eneo la mapigano”. Bunge la Ethiopia lilirefusha mwanzoni mwa Februari kwa miezi minne hali ya hatari iliyotangazwa mnamo Agosti 2023 huko Amhara ili kujaribu - bila mafanikio kwa sasa - kupunguza uasi wa Fano, uliochochewa na jaribio la serikali ya shirikisho kuwapokonya silaha vikosi vya Amhara.

Takriban 90% ya wakazi wa jimbo la Amhara takriban milioni 23 ni wa jamii ya Amhara. Tangu Abiy Ahmed awe Waziri Mkuu mwaka 2018, maeneo mengi ya Ethiopia, nchi ya pili kwa watu wengi zaidi barani Afrika yenye wakazi milioni 120, yamekumbwa na vurugu za kisiasa na/au za kijamii, zikiambatana na dhuluma nyingi zinazofanywa na kambi mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.