Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-USALAMA

Mandamano yatawanywa vibaya na vikosi vya usalama Dakar

Vikosi vya usalama vimetawanya maandamano ya raia mjini Dakar siku ya Ijumaa, kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais wakati wa siku ya majaribio ya kuonysha nguvu kati ya mamlaka ya Rais Macky Sall, mashirika ya kiraia na upinzani.

Waandamanaji wa Senegal waandamana kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais wa Februari 25, huko Dakar, Februari 9, 2024.
Waandamanaji wa Senegal waandamana kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais wa Februari 25, huko Dakar, Februari 9, 2024. REUTERS - ZOHRA BENSEMRA
Matangazo ya kibiashara

 

Makundi ya watu wakliojaribu kukaribia eneo kubwa la Place de la Nation yamezuiliwa na polisi waliotumia gesi ya kutoa machozi. Waandamanaji kadhaa walijibu kwa kurusha mawe. barabara zote zinazoelekea kwenye eneo hilo zimefungwa, waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP wamebaini.

Hali inasikitisha, tulikuja kusali tukarushiwa gesi, jambo ambalo halivumiliki. Wasenegal lazima waghadhibishwe na sio tu kwenye mitandao ya kijamii,” mmoja wa wagombea urais, Thierno Alassane Sall, ameliambia shirika la habari la AFP.

Uhamasishaji huu ni maandamano makubwa ya kwanza tangu kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais uliopangwa awali Februari 25, ambao ulifungua mzozo mkubwa wa kisiasa nchini Senegal na kuiingiza nchi hiyo katika kipindi cha sintofahamu.

Majaribio ya kuandamana tangu kutangazwa kwa kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais yamekandamizwa na makumi ya watu kukamatwa.
Majaribio ya kuandamana tangu kutangazwa kwa kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais yamekandamizwa na makumi ya watu kukamatwa. AFP - GUY PETERSON

Katika msikiti wa Masjid Nur huko Dakar, kwa ajili ya Swala kuu ya Ijumaa kwa Waislamu, ni waumini wachache tu waliokuwa wamevalia mavazi meupe na ya mavazi yenye rangi ya taifa, kwa wito wa muungano mpya ya mavuguvugu ya kiraia, makundi ya kidini na mashirika ya kitaaluma ambayo yanapinga kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais.

Lakini katika mahubiri yake, imam Ahmed Dame Ndiaye alipinga hali ya kisiasa. "Hata rais anaweza kufanya makosa na katika kesi hii ni juu yetu kumwambia ukweli," amesema, na kuongeza kuwa "hakuna mtu anye haki ya kutazama jamii ikiharibiwa".

Naye Mtoa adhana Souleymane Ndiaye amesema, Rais Macky Sall "amekataa na ni aibu kwa Wasenegali wote. Neno lililotolewa ni takatifu."

 

Kundi la wagombea kadhaa wa upinzani wamewasilisha rufaa katika Mahakama ya Juu siku ya Ijumaa mchana. Majaribio ya kuandamana tangu kutangazwa kwa kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais yamekandamizwa na makumi ya watu kukamatwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.