Pata taarifa kuu

Senegal: Wagombea wa upinzani wapinga kuahirishwa kwa uchaguzi

Nairobi – Wagombea 13 wa kiti cha urais wa upande wa upinzani nchini Senegal wameungana na kupinga hatua ya bunge kuahirisha uchaguzi hadi Desemba 15 mwaka huu, hatua ambayo wamesema ni mapinduzi ya kikatiba.

Wanasiasa hao wameshutumu hatua hiyo ambayo wamesema ni mapinduzi ya kikatiba
Wanasiasa hao wameshutumu hatua hiyo ambayo wamesema ni mapinduzi ya kikatiba AFP - JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Ni wagombea 13 kati ya 20 walioko kwenye orodha ya mwisho iliyoidhinishwa na mahakama ya kikatiba ya Senegal, ambao ni wanasiasa wa upinzani miongoni mwao, Amadou Ba, mwakilishi wa mgombeaji wa zamani wa Pastef Bassirou Diomaye Faye, wabunge Déthié Fall na Thierno Alassane Sall pia waziri wa zamani Aly Ngouille Ndiaye ambao wameungana pamoja ambapo wameshutumu hatua ya Bunge la taifa kuahirisha uchaguzi uliokuwa ufanyike tarehe 25 mwezi huu hadi tarehe 15 desemba.

Wanasiasa hao wameshutumu hatua hiyo ambayo wamesema ni mapinduzi ya kikatiba.

Akizungumza wakati wa kikao cha hapo jana waziri wa zamani Aly Ngouille Ndiaye amesema Wagombea hao ambao pia ni wabunge watawasilisha rufaa nyingine haraka iwezekanavyo katika Baraza la Katiba kupinga sheria iliyopitishwa Jumatatu ambayo inaahirisha uchaguzi hadi Desemba 15.

Jumuia ya maendeleo ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imewataka serikali ya Senegal kuheshimu uhuru wa watu kukusanyika na kujieleza, pia kuzingatia tamaduni za demokrasia za taifa hilo la Afrika Magharibi

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.