Pata taarifa kuu

Ecowas imekutana kujadili mzozo wa kisiasa nchini Senegal

Nairobi – Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imekutana kwa dharura siku ya Alhamisi, kujadili hali ya mzozo wa kisiasa nchini Senegal na tofauti kubwa iliyotokea hivi karibuni na tawala za kijeshi huko Burkina Faso, Mali na Niger.

Ecowas pia imejadili  hali ya mzozo wa kisiasa nchini Senegal na tofauti kubwa iliyotokea hivi karibuni na tawala za kijeshi huko Burkina Faso, Mali na Niger.
Ecowas pia imejadili hali ya mzozo wa kisiasa nchini Senegal na tofauti kubwa iliyotokea hivi karibuni na tawala za kijeshi huko Burkina Faso, Mali na Niger. REUTERS - FRANCIS KOKOROKO
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano wao wa hapo jana, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama za jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) waliokutana katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, wamesema kuwa mataifa ya Burkina Faso Mali na Niger, hayakuheshimu sheria katika kujiondoa katika jumuia hiyo.

Rais wa baraza kuu la ECOWAS linaloshughulikia masuala ya kisiasa, Omar Touray, amefahamisha kuwa uamuzi wa ghafla wa nchi hizo tatu haukufuata masharti yaliyowekwa ya kujiondoa, kwa sababu kila taifa mwanachama, kabla ya kujiondoa linapaswa kuwasilisha barua mwaka mmoja kabla.

Mkutano huo pia umejadili mzozo wa kisiasa unaoikumba nchi ya Senegal baada ya bunge la nchi hiyo kuahirisha uchaguzi wa rais hadi desemba 15 mwaka huu, hatua ambayo imezusha wasiwasi wa kutokea machafuko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.