Pata taarifa kuu

Ghana: Watu sita wahukumiwa kifo kwa kupanga jaribio la mapinduzi

Nairobi – Raia wawili wa Ghana wakiwemo wanajeshi watatu wamehukumiwa kifo kwa kuonyongwa kutokana na mchango wao katika kupanga mapinduzi ya kijeshi miaka mitatu iliopita.

Hii ilikuwa kesi ya kwanza ya uhaini nchini Ghana tangu kuangushwa kwa utawala wa Kwame Nkrumah mwaka wa 1966
Hii ilikuwa kesi ya kwanza ya uhaini nchini Ghana tangu kuangushwa kwa utawala wa Kwame Nkrumah mwaka wa 1966 © FMM
Matangazo ya kibiashara

Hii ilikuwa kesi ya kwanza ya uhaini nchini Ghana tangu kuangushwa kwa utawala wa Kwame Nkrumah mwaka wa 1966.

Sita hao walikamatwa mwaka wa 2021 wakati wakifanyia silaha majaribio jijini Accra wakidai kuwa na njama ya kuangusha serikali.

Washukiwa hao walikana kuhusika na njama hizo za mapinduzi wakati wa kusikilizwa kwa mashtaka dhidi yao.

Mawakili wao wamesema wakata rufa dhidi ya uamuzi huo katika mahakama ya rufa.

Watu wengine watatu akiwemo afisa wa ngazi ya juu wa polisi na wanajeshi wawili walifutiwa mashtaka.

Mahakama iliwakuta sita hao na makosa ya uhaini wa hali ya juu pamoja na njama ya kutekeleza uhaini mkubwa.

Walikamatwa wakiwa na bunduki za kujitengeneza, vilipuizi silaha nyengine kwa mujibu wa stakabadhi za mahakama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.