Pata taarifa kuu
ULINZI-USALAMA

Tisa waangamia katika shambulio kaskazini mashariki mwa Ghana

Watu tisa wameuawa katika shambulio lililotekelezwa na watu wasiojulikana Kaskazini-mashariki mwa Ghana mnamo Septemba 21, 2023. Shambulio hilo linakuja wakati wa mivutano ya kijamii. Waziri wa Ulinzi wa Ghana ametangaza kwamba machafuko ya kijamii yananufaisha makundi ya wanajihadi yaliopo katika eneo hilo.

Ramani ya Ghana.
Ramani ya Ghana. © FMM
Matangazo ya kibiashara

Shambulio la watu wasiojulikana wenye silaha limesababisha vifo vya watu 9 na wengine kadhaa kujeruhiwa nchini Ghana. Washambuliaji waliyafyatulia risasi magari mawili yaliyokuwa yamewabeba wafanyabiashara waliokuwa wakienda kwenye soko kubwa nchini Togo.

Shambulio hilo la kuvizia lilifanyika Septemba 21, 2023 katika wilaya ya Pusiga kaskazini mashariki mwa nchi, karibu na mpaka wa Burkina Faso, inayokabiliwa na uasi wa kijihadi. Wengi wa waathiriwa ni wanawake, kulingana na afisa wa eneo hilo.

Katika hatua hii, ni vigumu kuwatambua washambuliaji. Polisi ipo katika eneo la tukio na mkuu wa wilaya ya Pusiga ametangaza kuwa uchunguzi umefunguliwa ili kujaribu kubaini sababu za shambulio hili. Hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulio hili.

Kipindi cha mivutano ya kijamii

Shambulio hili linakuja wakati wa mvutano wa kijamii kati ya makabila ya Kusasi na Mamprusi, katika eneo la Bawku, karibu na mpaka na Burkina Faso.

Mvutano huu uliongezeka mwezi Februari mwaka jana wakati afisa wa uhamiaji aliuawa na wenzake wawili kujeruhiwa. Wakati huo huo, mamlaka ya Ghana ilituma wanajeshi 1,000 kwenye mpaka na Burkina Faso kulinda eneo hilo.

Kwa hakika, wachambuzi wanasema maafisa wa uhamiaji nchini Ghana leo wanatumia muda mwingi kukabiliana na machafuko ya makabila kuliko kulinda mipaka. Jambo ambalo linafanya maeneo ya mipaka kukabiliwa na mashambulizi ya kigaidi.

Ukweli kwamba washambuliaji wamewashambulia raia wanaokwenda sokoni unaonyesha, kwa baadhi ya wataalam, kuhusika kwa wanajihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.