Pata taarifa kuu

Nigeria: Ushawishi wa wainjilisti uliokosolewa baada ya shutuma dhidi ya Mchungaji TB Joshua

Enzi za uhai wake, mchungaji mashuhuri wa Nigeria TB Joshua alifuatwa na maelfu ya wafuasi ndani na nje ya nchi, waliomiminika kushuhudia miujiza yake.

TB Joshua, aliyepewa jina la utani "Nabii", hata hivyo, hakukubaliwa kwa kauli moja ndani ya makanisa ya kiinjili, tawi la Uprotestanti. Mnamo mwezi Aprili 2021, YouTube iliondoa chaneli yake baada ya kudai kutibu ushoga, jambo ambalo ni kinyume cha sheria nchini Nigeria.
TB Joshua, aliyepewa jina la utani "Nabii", hata hivyo, hakukubaliwa kwa kauli moja ndani ya makanisa ya kiinjili, tawi la Uprotestanti. Mnamo mwezi Aprili 2021, YouTube iliondoa chaneli yake baada ya kudai kutibu ushoga, jambo ambalo ni kinyume cha sheria nchini Nigeria. AFP/File
Matangazo ya kibiashara

 

Lakini mwinjilisti huyo wa Kikristo, ambaye alikufa ghafla akiwa na umri wa miaka 57 mnamo mwaka 2021, pia anatuhumiwa kwa mateso, unyanyasaji wa kijinsia, ubakaji na ulaghai. Leo, kanisa lake la kiinjili, Kanisa la Synagogue Church of All Nations (Scoan), lililoko Lagos, mji mkuu wa uchumi wa nchi hiyo na jiji lenye watu wengi zaidi barani, kwa mara nyingine tena ni linalegwa na shutuma za unyanyasaji.

Katika mfululizo wa video na makala zilizochapishwa mnamo mwezi wa Januari, BBC ilitoa ushuhuda zaidi ya ishirini kutoka kwa wafuasi wa zamani wa Scoan wakiripoti unyanyasaji na miujiza iliyoigizwa na TB Joshua, ambaye jina lake halisi ni Temitope Balogun Joshua. Scoan ilikanusha madai hayo haraka, ikisema hakuna hata mmoja wa watu wanaoonekana kwenye video hizo ambaye ni waumini wa kanisa hilo.

Nchini Nigeria, shutuma hizi zinaangazia uwezo wa baadhi ya wachungaji wa kiinjilisti, pamoja na ukosoaji unaolengwa kwao huku utendaji wa ndani wa makanisa yao ukiendelea kuwa wazi, kulingana na wataalamu waliohojiwa na shirika la habari la AFP.

"Kosa ambalo halitakiwi kufanyika ni kuzingatia TB Joshua. Somo halisi ni ushawishi wa wachungaji na jinsi wanavyoutumia," amesema Ebenezer Obadare, anayehusika na uchunguzi barani Afrika katika shirika la Think Tank Council on Foreign Relations na mwandishi wa Pastoral Power, Jimbo la Makasisi: Upentekoste, Jinsia na maumbile nchini Nigeria. "Kiongozi wa kiume ni mkuu na waamini wote wako chini ya mchungaji wa Kipentekoste, ambaye ana nguvu nyingi za kisiasa na kiuchumi lakini pia nguvu za mapenzi," anaongeza.

Baada ya machapisho ya BBC, watumiaji wa mtandao walienda kwa fujo kwenye mitandao ya kijamii, huku watu wengi wakiwashutumu mashahidi na vyombo vya habari vya Uingereza kwa kutaka kudhuru urithi wa mchungaji huyo.

Watu wenye nguvu

Nchini Nigeria, nchi yenye uhafidhina wa kidini iliyogawanyika kati ya kaskazini yenye Waislamu wengi na kusini yenye Wakristo wengi, wachungaji wana ushawishi mkubwa. TB Joshua, aliyepewa jina la utani "Nabii", hata hivyo, hakukubaliwa kwa kauli moja ndani ya makanisa ya kiinjili, tawi la Uprotestanti. Mnamo mwezi Aprili 2021, YouTube iliondoa kituo chake baada ya kudai kutibu ushoga, jambo ambalo ni kinyume cha sheria nchini Nigeria.

Pia alijivunia kuwa ameponya watu wa UKIMWI na kudai kwamba janga la UVIKO-19 lingeisha Machi 27, 2020. Viongozi wa makanisa ya Nigeria kwa muda mrefu wamekuwa wakitoa tahadhari kuhusu tabia yake.

Mnamo mwaka wa 2009, Pentecostal Fellowship of Nigeria (PFN), mojawapo ya makundi makubwa ya Kikristo ya kiinjilisti nchini, ilijitenga hadharani na kanisa la TB Joshua, na kumtaka "kutubu" na "kugeukia" Ukristo. Ayo Oritsejafor, kiongozi wa PFN wakati huo, alimshutumu TB Joshua kwa kufanya kazi ya uchungaji bila kupata mafunzo ya awali.

Hadi kifo chake Juni 2021, Joshua na wahandisi wawili walikuwa chini ya mashtaka ya uzembe wa jinai katika mahakama ya Lagos kufuatia tukio la Septemba 2014 la kuanguka kwa nyumba ya wageni ya ghorofa sita iliyokuwa ikijengwa kwenye uwanja wa kanisa lake, na kusababisha vifo vya watu 116, wengi wao Waafrika Kusini. Msemaji wa Wizara ya Sheria ya Jimbo la Lagos hakujibu maswali ya shirika la habari la AFP kuhusu hali ya kesi hii.

Kulingana na Babatomiwa Owojaiye, mwanzilishi wa Kituo cha Ukristo wa Kibiblia Barani Afrika, Waafrika wengi waliamini miujiza yake licha ya shutuma dhidi yake. Anaona kuwa ni vigumu kudhibiti shughuli za wanaojiita manabii na viongozi wa kidini kwa vile hawahusiani na muundo rasmi ambao utafanya kazi kama ulinzi.

Katika mengi ya makanisa haya, unyanyasaji mwingi unafanywa bila kudhibitiwa na yeyote anayezungumza ni mwathirika wa vitisho, wizi, kudhulumiwa, kutengwa au kunyamazishwa,” ameliambia shirika la habari la AFP. "Lakini mashitaka haya hayatoshi kuwataja wainjilisti wote wa Nigeria kuwa ni wanafiki na wanajihusisha na vitendo vya kikatili.

Msemaji wa PFN Emmah Isong ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kundi hilo limeonya mara kwa mara dhidi ya TB Joshua, bila kutetereka uungwaji mkono wa mchungaji. “Tumeshutumiwa kuwa tuna wivu na uwaziri wa mtu huyu, tusitupiwe virago kwa kuusimamia ukweli,” amesisitiza.

Mnamo Januari 26, Mahakama ya Haki ya Lagos ilimhukumu mchungaji mwingine wa kiinjilisti, Oluwafeyiropo Daniels, kifungo cha maisha jela kwa kosa la ubakaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.