Pata taarifa kuu

Basi la shule lavamiwa na watekaji nyara nchini Nigeria

Machifu wawili wa kimila waliuawa na watoto watano na walimu wao kutekwa nyara siku ya Jumatatu katika mashambulizi tofauti katika Jimbo la Ekiti, kusini magharibi mwa Nigeria, nchi ambayo ukosefu wa usalama unasababisha kuongezeka kwa ghadhabu, kulingana na vyanzo vya polisi.

Habari ya Kutekwa nyara kwa wasichana 276 wa shule huko Chibok, kaskazini mashariki mwa Nigeria, na wanajihadi wa Boko Haram iligonga vichwa vya habari mwaka 2014.
Habari ya Kutekwa nyara kwa wasichana 276 wa shule huko Chibok, kaskazini mashariki mwa Nigeria, na wanajihadi wa Boko Haram iligonga vichwa vya habari mwaka 2014. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Utekaji nyara kwa ajili ya fidia unaofanywa na magenge ya wahalifu ni tatizo kubwa nchini Nigeria na serikali mpya ya Rais Bola Ahmed Tinubu, aliyeingia madarakani mwezi Mei 2023, inakabiliwa na ukosoaji mkubwa baada ya mfululizo wa visa vya utekaji nyara vya hivi majuzi.

Siku ya Jumatatu, watu wenye silaha walishambulia basi la shule na kuwateka nyara watoto watano na walimu wao karibu na mji wa Emure katika jimbo la Ekiti, kulingana na mwanzilishi wa shule na polisi. Walipiga risasi matairi ya basi na kuwateka nyara wanafuzi hao waliokuwa wakitoka shuleni, Gabriel Adesanya, mwanzilishi mwenza wa shule hiyo, ameliambia shirika la habari la AFP.

Amesema wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Emure Apostolic Faith, wenye umri wa miaka 8 hadi 14, bado hawajulikani walipo, pamoja na dereva wa basi, kondakta na walimu wawili. "Sijawahi kuona kitu kama hiki hapo awali, wazazi wana wasiwasi sana," amesema.

Polisi imethibitisha kisa hiki cha utekaji nyara kwa shirika la habari la AFP na kusema wametuma maafisa "kuhakikisha watu hao wanaokolewa na washukiwa kukamatwa". Polisi imeliambia shirika la habari la AFP kwamba watawala wawili wa kimila kutoka jimbo moja - Onimojo wa Imojo-Ekiti, Oba Olatunde Samuel Olusola, na Elesun wa Esun-Ekiti, Oba David Babatunde Ogunsol - waliuawa siku moja na watu wasiojulikana.

Katika taarifa iliyowasilishwa na msemaji wake siku ya Jumanne, Rais Bola Ahmed Tinubu ameelezea masikitiko yake kwa familia za viongozi hawa wawili wa eneo hilo na kutoa wito wa "kuokolewa mara moja" kwa watoto wa shule na walimu waliotekwa nyara.

Bw. Tinubu aliingia madarakani mwaka jana na kuahidi kukabiliana na ukosefu wa usalama nchini Nigeria, wakiwemo wanajihadi kaskazini mashariki, wanamgambo wahalifu kaskazini magharibi na kuongezeka kwa ghasia kati ya jamii katikati mwa nchi.

Shirika la Ujasusi la Nigeria la SBM Intelligence limesema kuwa limerekodi watu 3,964 waliotekwa nyara nchini Nigeria tangu Tinubu aingie madarakani. Habari ya Kutekwa nyara kwa wasichana 276 wa shule huko Chibok, kaskazini mashariki mwa Nigeria, na wanajihadi wa Boko Haram iligonga vichwa vya habari mwaka 2014

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.