Pata taarifa kuu

Kipindi cha hali ya hatari chaongezwa katika jimbo la Amhara nchini Ethiopia

Wabunge wa Ethiopia siku ya Ijumaa wameongeza muda wa hali ya hatari tangu mwezi Agosti katika jimbo la Amhara, ambalo ni la pili kwa idadi kubwa ya watu nchini Ethiopia, ambapo wanamgambo wa eneo hilo wamechukua silaha kwa karibu mwaka mmoja dhidi ya jeshi la shirikisho.

Wanamgambo wa Amhara, wakati huo washirika wa jeshi la shirikisho dhidi ya waasi wa Tigray, wanapewa mafunzo karibu na Addis Zemen, Novemba 10, 2020.
Wanamgambo wa Amhara, wakati huo washirika wa jeshi la shirikisho dhidi ya waasi wa Tigray, wanapewa mafunzo karibu na Addis Zemen, Novemba 10, 2020. © AFP / EDUARDO SOTERAS
Matangazo ya kibiashara

 

"Baada ya kusikiliza maelezo ya Waziri wa Sheria Gedion Timotheos ambaye aliwasilisha azimio hilo," Baraza la Wawakilishi la Wananchi "limeidhinisha" kurefushwa kwa kipindi cha hali ya hatari katika jimbo la kaskazini la Amhara, baraza la Wawakilishi limesema katika taarifa yake iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Taarifa hiyo haielezei muda wa kurefushwa kwa kipindi hiki lakini hauwezi kuzidi miezi minne, kwa mujibu wa Katiba ya nchi ya pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika. Ibara ya 93 inasema kwamba hali ya hatari inatangazwa hapo awali kwa miezi sita, na baada ya hapo Wabunge wataidhinishwa tu kurefusha kwa vipindi mfululizo vya miezi minne.

Azimio, ambalo lilikuwa lipate thuluthi mbili ya kura za wabunge, "limeidhinishwa kwa wingi wa kura, na kura mbili tu za kupinga na tatu wabunge watatu wamejizuia", linabainisha Baraza la Wawakilishi ambaclo Chama cha Waziri Mkuu, Abiy Ahmed , kina zaidi ya 95% ya viti.

Kuanzishwa kwa hali ya hatari huko Amhara miezi sita iliyopita kumeshindwa kuzima uasi wa wanamgambo wa kujilinda wa FANO, maarufu Amhara, na kurejesha utulivu katika eneo hilo. Wafano, kama Waamhara wengi, wanahisi kusalitiwa na makubaliano ya amani yaliyotiwa saini na Abiy Ahmed mnamo mwezi wa Novemba 2022 na viongozi wasiokubalika wa eneo jirani la Tigray, maadui wa muda mrefu wa wanataifa wa Amhara ambao wanadai "ardhi ya mababu" inayohusishwa na Tigray kiutawala.

Wakati wa miaka miwili ya vita huko Tigray, vikosi vya Amhara vilisaidia jeshi la shirikisho dhidi ya waasi wa Tigray na mnamo mwezi wa Aprili 2023, jaribio la serikali ya shirikisho la kuvipokonya silaha vikosi vya FANO na Amhara lilichochea uhasama Amhara. Tangu wakati huo, Wafano wameongeza operesheni za waasi dhidi ya jeshi la serikali na waliweza katika miezi ya hivi karibuni kudhibiti kwa kipindi kifupi maeneo muhimu, kama vile Gondar, mji mkuu wa zamani wa kifalme, au jiji takatifu la Lalibela.

Hali ya hatari nchini Ethiopia inahamisha jukumu la usalama kwa "Machapisho ya Amri" ya kijeshi na kusimamisha idadi ya haki na uhuru. Hasa, inawezesha kukamatwa na kufanya upekuzi bila hati na kupanua misingi na vipindi vya kizuizini bila uamuzi wa mahakama. Inatumika katika jimbo la Amhara, lakini pia inahusu kwenye ardhi yote ya Ethiopia mtu yeyote anayeshukiwa kuhusika na vurugu katika eneo hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.