Pata taarifa kuu

Mashambulizi mawili katikati mwa Nigeria yauwa zaidi ya watu 50

Mashambulizi mawili kaskazini-kati mwa Nigeria kati ya Jumanne na Jumatano yaligharimu maisha ya watu 55, kwa mujibu wa viongozi wawili wa jamii na ripoti ya Shirika la Msalaba Mwekundu la Nigeria ambayo shirika la habari la AFP limepata kopi siku ya Alhamisi.

Gari la polisi linaonekana katika kitongoji cha Zabarmari karibu na Maiduguri mnamo Novemba 6, 2023.
Gari la polisi linaonekana katika kitongoji cha Zabarmari karibu na Maiduguri mnamo Novemba 6, 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Licha ya sheria ya kutotoka nje iliyotangazwa siku ya Jumanne katika wilaya ya Mangu, shule, maeneo ya ibada na nyumba zilichomwa moto wakati wa mashambulizi yote mawili, viongozi wa jamii wamesema.

Mwaghavul Development Association, shirika linalowaleta pamoja watu wa kabila la Mwaghavul, hasa Wakristo, limeshutumu wafugaji kutoka jamii ya Waislamu wa Fulani kwa kushambulia kijiji cha Kwahaslalek na kuua "takriban watu 30".

Idadi hii imethibitishwa na afisa wa misaada wa eneo hilo na chanzo cha misaada ya kibinadamu, ambao wamezungumza na shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina. Wasemaji wa polisi na jeshi hawakujibu mara moja maombi ya AFP ya kuthibitishwa kwa habari hii.

"Kambi mbili za watu waliokimbia makazi zimeanzishwa katika mji wa Mangu, kwa watu wapatao 1,500," Nurudeen Husaini Magaji, mkuu wa shirika la Msalaba Mwekundu nchini Nigeria katika eneo hilo, ameliambia shirika la habari la AFP.

Gavana wa Plateau alitangaza amri ya kutotoka nje siku ya Jumanne baada ya makabiliano mapya ambayo mamlaka ilihusisha na mzozo kati ya mfugaji kuhamisha ng'ombe wake na wakazi wengine wanaotumia barabara. Shambulio la pili lilifanyika katika mji wa Mangu pia kati ya Jumanne na Jumatano.

Jumuiya ya Waislamu ya Jama'atu Nasril Islam (JNI), imesema maeneo ya ibada na shule yalishambuliwa.

"Tulipata maiti 25, tunasubiri ulinzi wa vikosi vya usalama ili kuzika," Jafaru Musa, mmoja wa viongozi wa eneo la JNI, ameliambia shirika la habari laAFP kwa simu.

"Tunaendelea na msako wetu kwa msaada wa Shirika la Msalaba Mwekundu ili kuona kama bado tunaweza kupata waliokufa, kwa sababu watu wengi wametoweka," ameongeza. Ripoti hii imethibitishwa na ofisa mwingine wa JNI, Salim Musa.

Mashambulizi ya mara kwa mara

Jimbo la Plateau, lililo kwenye mstari unaogawa kaskazini mwa Nigeria wenye Waislamu wengi na Kusini wenye Wakristo wengi, ni kitovu cha vurugu kati ya jamii hizi mbili.

Mvutano umeongezeka tangu karibu watu 200 kuuawa wakati wa Krismasi katika uvamizi kwenye vijiji vyenye Wakristo.

Mapigano katika majimbo ya kaskazini-magharibi na kaskazini-kati ya Nigeria yanatokana na mivutano ya jamii hizi mbili kuhusu matumizi ya ardhi kati ya wafugaji wa kuhamahama na wakulima wasio na shughuli. Lakini aina hizi za mashambulizi zimeongezeka na kuwa uhalifu mpana.

Tangu aingie madarakani mwezi Mei, Rais Bola Ahmed Tinubu amesema vita dhidi ya ukosefu wa usalama ni kipaumbele, hasa kwa nia ya kuvutia wawekezaji wa kigeni nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.