Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Gabon: Watu wenye silaha wavamia nyumba ya Mwenyekiti wa ECCAS, Gilberto da Piedade

Mwishoni mwa mkutano wa mwisho wa ECCAS (Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati), Gabon ilimwita balozi wake nchini Angola. Mwanadiplomasia huyo bado hajarejea Luanda kufuatia mtazamo unaochukuliwa kuwa si wa kirafiki kwa Angola dhidi ya mamlaka ya mpito ya Gabon. 

Wakati wa mkutano wa mwisho wa ECCAS mnamo Desemba 15 huko Equatorial Guinea, Angola ilisemekana kuwa haikuwezaa kuonyesha ushirikiano kuhusu utekelezwaji wa vikwazo dhidi ya Gabon.
Wakati wa mkutano wa mwisho wa ECCAS mnamo Desemba 15 huko Equatorial Guinea, Angola ilisemekana kuwa haikuwezaa kuonyesha ushirikiano kuhusu utekelezwaji wa vikwazo dhidi ya Gabon. © CEEAC
Matangazo ya kibiashara

 

Na mwandishi wetu wa Libreville, Yves Laurent Goma

Siku ya Alhamisi Januari 17, nyumba ya mwenyekiti wa Tume ya ECCAS ilishambuliwa huko Libreville na "watu wenye silaha, ambao baadhi yao walikuwa wamevalia sare za jeshi la Gabon". Luanda inadai "maelezo" kutoka kwa mamlaka ya Gabon.

Kulingana na tukio hili lililosimuliwa na mwenyekiti wa Tume ya ECCAS katika maelezo yake, watu watano waliingia katika makazi yake licha ya upinzani kutoka kwa walinzi. Ilikuwa saa 3:30  asubuhi. Gilberto da Piedade Verissimo, raia wa Angola, hakuwa nyumbani. Vyumba vyote vilipekuliwa. Milango ilivunjwa.

Saa 9:00 alaasiri, watu hao wenye silaha walirejea katika makazi ya Gilberto da Piedade Verissimo. Wakati huo, Mwenyekiti wa Tume ya ECCAS alikuwepo. Jenerali huyu wa jeshi la Angola alitishiwa binafsi.

Siku iliyofuata, Mwenyekiti wa Tume ya ECCAS aliwasiliana na serikali ya Gabon kupitia ujumbe mfupi wa maneno. Libreville mara moja ilituma maafisa wa polisi kwenye eneo la tukio na kufungua uchunguzi. Mara moja Luanda ilimwita Balozi mdogo wa Gabon nchini Angola kupata maelezo.

Uhusiano kati ya Gabon na Angola hauko katika hali nzuri. Rais wa Angola pia ndiye rais pekee wa Afrika ya Kati ambaye hajmpokea rais wa kipindi cha mpito cha Gabon. Wakati wa mkutano wa mwisho wa ECCAS mnamo Desemba 15 huko Equatorial Guinea, Angola ilisemekana kuwa haikuwezaa kuonyesha ushirikiano kuhusu utekelezwaji wa vikwazo dhidi ya Gabon

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.