Pata taarifa kuu

Macron azuru nchi tatu za Afrika ya Kati siku ya Ijumaa

Miji mikuu mitatu ndani ya saa chache kwa "uhusiano mpya" na Afrika: Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaendelea na ziara yake katika nchi za ukanda wa Afrika ya Kati leo Ijumaa. Ziara iliyonuiwa kuonyesha sura mpya ya diplomasia ya Ufaransa katika bara la Afrika.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto) akutana na rais wa Angola Joao Lourenço katika ikulu ya Casa Rosada, huko Luanda mnamo Machi 3, 2023.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto) akutana na rais wa Angola Joao Lourenço katika ikulu ya Casa Rosada, huko Luanda mnamo Machi 3, 2023. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa aliwasili Alhamisi jioni nchini Angola kutoka Gabon ambako alihudhuria mkutano wa kilele wa uhifadhi wa misitu ya kitropiki. Siku ya Ijumaa, mtawalia atakutana na mwenzake wa Angola Joao Lourenço mjini Luanda kisha Rais wa Congo Denis Sassou Nguesso mjini Brazzaville, kabla ya kuelekea Kinshasa jioni, hatua ya mwisho katika ziara yake.

"Nchini Gabon kama kwingineko, Ufaransa ni mpatanishi asiyeegemea upande wowote," rais Macron alisema, huku upinzani wa Gabon ukimshutumu kwa kumuunga mkono rais Ali Bongo Ondimba, aliyemrithi babake Omar Bongo Ondimba, katikati ya mwaka wa uchaguzi.

Nchini Angola, koloni la zamani la Ureno ambapo mtangulizi wake François Hollande alitembelea mwaka 2015, kazi bila shaka itakuwa rahisi. Emmanuel Macron, ambaye ana hamu ya kubadilisha uhusiano wa Ufaransa na bara hilo, ameongeza ziara zake katika nchi zisizozungumza Kifaransa tangu muhula wake wa kwanza (2017-2022).

'Utaalam'

Huko Luanda, makubaliano ya ushirikiano lazima yakamilishwe ili kuimarisha sekta ya kilimo ya nchi hii na kuleta mseto wa uchumi wake, ambao umejikita zaidi katika uzalishaji wa mafuta.

Angola, ambayo inaagiza kutoka nje sehemu kubwa ya bidhaa zake za chakula, inataka kuimarisha "uhuru" wake katika suala hilo na "kutafuta vyanzo vipya vya mapato katika sekta ya kilimo", Ikulu ya Elysée imebainisha. Ufaransa inaweza kutoa "maarifa" kwa sekta kutoka kwa uzalishaji hadi usindikaji na uuzaji, imeongeza.

Rais wa Ufaransa ataambatana na wawakilishi wa makampuni makubwa ya nafaka, wataalamu wa maendeleo ya miundombinu kama vile Meridiam na Total, ambayo iko nchini Angola katika uzalishaji wa hidrokaboni lakini pia katika umeme na maji safi.

Rais wa Angola, ambaye kuchaguliwa kwake tena mwaka 2022 kulipingwa na upinzani, ni sehemu ya mwendelezo wa Chama cha Popular Movement for the Liberation of Angola (MPLA), madarakani tangu uhuru mwaka 1975 na kwa muda mrefu chama kimoja.

Emmanuel Macron atasimama kwa saa chache Brazzaville ambako Denis Sassou Nguesso ametawala kwa mkono wa chuma kwa karibu miaka 40. Katika mkesha wa kuwasili kwake, mashirika ya haki za binadamu ya Kongo yalielezea wasiwasi wao na kumwomba rais wa Ufaransa kuyawasilisha.

"Tusubiri kwa Amani"

Waliomba kuachiliwa kwa Jenerali Jean-Marie Michel Mokoko na André Okombi Salissa. Mtawalia mkuu wa zamani wa majeshi na waziri wa zamani, watu hawa wawili walihukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani baada ya uchaguzi wa urais wa 2016 ambao walishindwa na kupinga.

Emmanuel Macron kisha atasafiri kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, koloni la zamani la Ubelgiji ng'ambo ya Mto Kongo, kwa ziara inayozingatia ushirikiano katika masuala ya afya na utamaduni. Atatembelea Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Tiba ya Kijamii siku ya Jumamosi na kukutana huko na Profesa Jean-Jacques Muyembe, ambaye alihusika na ugunduzi wa virusi vya Ebola. Pia atakutana na wasanii na wajasiriamali kutoka ulimwengu wa utamaduni.

Hatua hii inaweza kuwa gumu kwani Ufaransa inashutumiwa nchini DRC kwa kuunga mkono Rwanda badala ya Kinshasa, ambayo inakabiliwa na uasi mashariki mwa nchi hiyo. Vijana kadhaa, wakipeperusha bendera za Urusi, waliandamana kupinga kuwasili kwake Kinshasa siku ya Jumatano. Alhamisi, dazeni kati yao walichoma bendera ya Ufaransa mbele ya Taasisi ya Ufaransa huko Goma mashariki mwa nchi, alibainisha mwandishi wa shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.