Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Mtazamo na maoni juu ya hotuba ya Rais Macron kuhusu sera ya Ufaransa kwa Afrika

Kabla ya kuanza, Jumatano, Machi 1, ziara yake katika bara la Afrika ambayo itampeleka Gabon, Angola, Kongo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, alitangaza, Jumatatu hii, Februari 27, mwelekeo wa sera yake mpya kwa Afrika. Maoni ya kwanza yaliyokusanywa na RFI.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, alitangaza, Jumatatu hii, Februari 27, 2023, katika Ikulu ya Élysée mwelekeo wa sera yake ya Kiafrika kwa miaka ijayo.
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, alitangaza, Jumatatu hii, Februari 27, 2023, katika Ikulu ya Élysée mwelekeo wa sera yake ya Kiafrika kwa miaka ijayo. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Libreville, mji mkuu wa Gabon, ni hatua ya kwanza ya ziara hii ambapo yuko mwandishi wetu maalum Paulina Zidi.

"Ni majadiliano kabla ya mechi, kabla ya kuingia uwanjani", alitangaza Emmanuel Macron ili kubaini hotuba hii kuhusu ushirikiano wa baadaye wa Afrika na Ufaransa, hotuba ambayo alitaka kuitoa nchini Ufaransa kwa sababu inawahusu pia Wafaransa. Usizungumze kuhusu Afrika pekee barani Afrika, lakini hamasisha kabla ya ziara hii muhimi, aliongeza rais wa Ufaransa.

Nchi nne, katika siku nne - Gabon, Angola, Kongo-Brazzaville na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) - na mada nne: mapambano dhidi ya mabadiliko ya Tabia nchi na ulinzi wa misitu huko Libreville, usalama wa chakula huko Luanda, maswala ya kumbukumbu huko Brazzaville na hatimaye mazungumzo na mashirikiano ya kiuchumi, kisayansi na kitamaduni huko Kinshasa.

Mlolongo mrefu wa ziara hii ya 18ᵉ ya rais wa Ufaransa katika bara la Afrika, ya pili katika Afrika ya Kati katika muda wa miezi sita. "Nadhani ziara hii ni muhimu", aliongeza Emmanuel Macron, katika ukanda huu unaokumbwa na changamoto za usalama, lakini pia mazingira, afya na mengine.

Kitendo cha kusawazisha pia kwa rais wa Ufaransa ambaye anasafiri kwenda nchi mbili, Gabon na DRC, katikati ya mwaka wa uchaguzi, na uchaguzi wa rais umepangwa, mtawalia mwishoni mwa msimu wa joto na mwishoni mwa mwaka, jambo ambalo tayari limewafanya baadhi ya wapinzani na mashirika ya kiraia ya Gabon kuguswa, ambao wanadai kwamba ziara hii inaonekana  kumuunga mkono Rais Ali Bongo, ambaye anaweza kuwania tena muhula wa tatu.

Hotuba ya rais wa Ufaransa mjini Dakar

Nchini Senegal, mwanahabari wetu Charlotte Idrac alifuatilia hotuba hiyo na wanafunzi kutoka shule ya uandishi wa habari CESTI, katika Chuo Kikuu cha Cheikh Anta Diop huko Dakar.

Wanafunzi karibu ishirini walifuata kwa makini hotuba hii kwenye televisheni kubwa iliyounganishwa na France 24, moja kwa moj.

Hotuba ikifuatwa kwa makini. baadhi waliandika baadhi ya maneneo ya rais. Kulikuwa na tabasamu chache, miguno pia. Lakini kinachoonekana ni kwamba hotuba hii haikuwashawishi vijana hawa.

"Hakuna jipya", alisema mmoja wao ambaye alikuwa amefuatilia hotuba ya Ouagadougou mwaka wa 2017. Alisema alikuwa na hisia ya kusikia mambo yale yale, maneno yale yale, ahadi zilezile za mpasuko.

Usalama na ushirikiano

Kinshasa, mji mkuu wa DRC, ni moja ya hatua za ziara rasmi ya mkuu wa nchi wa Ufaransa. Akijumuika na RFI, Christophe Lutundula, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo, alibainisha mambo mbalimbali ya hotuba ya Emmanuel Macron, hasa masuala ya usalama na ushirikiano wa kiuchumi.

"Kwa upande wetu, DRC, ninaona kwa shauku kubwa mambo mawili ya msingi. Kwanza, Rais Macron anatambua kwamba Ufaransa inawajibika kwa mambo yaliyopita na kwamba hadi wakati huo, hakujawa na matokeo yoyote, kwa vyovyote vile, matokeo yaliyotarajiwa. "

"Pia kuna kipengele muhimu, kwa vyovyote vile, kwetu, DRC, ni kwamba alisisitiza umuhimu wa suala la usalama barani Afrika. Bila kuficha, nadhani kwamba msimamo wa Ufaransa dhidi ya Rwanda lazima uwe wazi. Ufaransa imeitaka Rwanda kusitisha uungaji wake mkono kwa M23, Ufaransa lazima pia izingatie namna Rwanda imepokea ujumbe huu, ombi hili na kuutumia. »

“Rais pia alizungumza kuhusu usaidizi katika ujasiriamali. Hii ni sura ambayo inatuvutia kwa sababu kwa kweli, hakuna maslahi ya Ufaransa, kwa vyovyote vile si muhimu, nchini DRC. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.