Pata taarifa kuu
KURA YA MAONI

Kura ya maoni ya katiba nchini Chad: kampeni yaingia kipindi cha lala salama

Wiki moja kabla ya kura ya maoni ya Katiba mpya nchini Chad, kambi za "Ndiyo" na "Hapana" zinatetea misimamo yao kwa hali na mali, huku wengine wakiamua kususia.

Muonekano wa angani wa mji wa Ndjamena.
Muonekano wa angani wa mji wa Ndjamena. © David Baché/RFI
Matangazo ya kibiashara

Kampeni ya kura ya maoni inapoingia wiki yake ya mwisho, wanasiasa wanatetea misimamo yao kabla ya kupiga kura ya Katiba mpya, uchaguzi uliyopangwa kufanyika siku ya Jumapili, Desemba 17. Huko Ndjamena, wikendi hii iliangaziwa na mikutano ya vyama tofauti vya kisiasa, anaripoti mwanahabari wetu Olivier Monodji.

Wanaharakati kutoka Patriotic Salvation Movement (MPS), chama tawala cha zamani, na vyama washirika vinavyounga mkono mpito tayari wanasema wana uhakika wa ushindi wao. "Kambi iliyo pinzani inaonyesha kuwepo kwa mgawanyiko wa Chad. Tunakwenda kwenye kura ya maoni kusema "Ndiyo", ili kuwezesha watu waendelee haraka kuweka utaratibu wa kikatiba. Mpigie kura Chad iliyoungana na isiyogawanyika,” amesema Mahamat Zen Bada Abbas, Naibu kiongozi wa muungano wa "Ndio" katika kura ya maoni ya katiba.

Kambi ya "Hapana" inasema iko tayari kupambana hadi mwisho

Lakini hii haiathiri kwa vyovyote uamuzi wa kambi ya "Hapana". "Msimamo wa serikali ya umoja umependelea uundaji wa maasi, mizozo, migogoro ya kijamii, vita. Na kwa hali hiyo haitufurahishi. Tunatoa wito wa kura ya "Hapana" dhidi ya Katiba inayopendekezwa ya umoja, kwa sababu propaganda hii dhidi ya shirikisho inawanufaisha," amesema Brice Mbaimon Guedmbaye, mratibu wa kitaifa.

Maandishi hayo, yaliyopitishwa mwezi Juni na Bunge la Mpito, yanastahili kuanzisha kurejea kwa utaratibu wa kikatiba na kukomesha mpito huo kufuatia kifo cha rais wa zamani Idriss Déby. Inachukua usanifu wa makubaliano ya sheria ya msingi ya mwaka 1996, na kwa swali kuu la muundo wa taifa, inaahidi ugatuaji wa hali ya juu badala ya shirikisho.

Kila siku bila kubadilika

Kwa upande wa Kundi la Ushauri la Watendaji wa Kisiasa (GCAP), muungano ambao unatetea kususia kura ya maoni, iwe tunapiga kura ya "Ndiyo" au "Hapana", hii haitabadilisha chochote kila siku. "Tulinde mustakabali wetu kwa kusema tukomeshe kura ya maoni. Kupiga kura kunamaanisha kukubali kuishi bila maendeleo ya kiuchumi. Ni lazima tufanye kila kitu kuzuia kura hii ya maoni,” amesema Nassour Ibrahim Koursami, kiongozi wa chama cha Les Patriotes, mwanachama wa GCAP. Wasiwasi wa Wachad upo mahali pengine, amesema. wasiwasi huo unahusu hasa kufungwa kwa shule kwa karibu miezi miwili na mafuta ambayo yanazidi kuwa haba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.