Pata taarifa kuu

Raia Chad kushiriki kura ya maoni kuhusu katiba mpya Jumapili ijayo

Raia wa Chad wanajiandaa kushiriki kwenye kura ya maoni siku ya Jumapili, kuamua iwapo wanaitaka katiba mpya au la.

Rais wa Chad Mahamat Idriss Déby wakati wa mkutano wa COP28 huko Dubai, Desemba 1, 2023.
Rais wa Chad Mahamat Idriss Déby wakati wa mkutano wa COP28 huko Dubai, Desemba 1, 2023. © AP - Rafiq Maqbool
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo itakuwa njia mojawapo ya kumaliza uongozi wa kijeshi, katika nchi ambayo kwa miaka 30 imekuwa ikiongozwa na família ya Deby.

Kikubwa kitakachoamuliwa ni kuhusu mfumo wa utawala nchini humo, ambapo kuna mapendekezo ya kuwa na serikali kuu au kuwe na serikali za majimbo.

Wapinzani wamekuwa wakitaka raia wa Chad, kuunga mkono mfumo wa uongozi wa majimbo, ili kuleta maendeleo nchini humo, wakisema mfumo wa sasa haujasaidia. Hata hivyo, baadhi ya wapinzani wameapa kususia zoezi hilo.

Baada ya kuuawa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo, Idriss Deby Itno mwaka 2021 na makundi ya waasi, mwanaye Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno, alichukua hatamu za uongozi na sasa anaiongoza Chad kwenye mchakato huo.

Baada ya kuchukua madaraka, aliahidi kuandaa uchaguzi baada ya miezi 18 lakini mwaka uliopita, alitangaza kuongeza kipindi cha mpito kwa miaka mingine miwili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.