Pata taarifa kuu

Guinea-Bissau: Jeshi linasema limethibiti hali baada ya kuripotiwa makabiliano mapema leo

Nairobi – Msemaji wa jeshi la Guinea-Bissau, Kapteni Jorgito Biague, amesema jeshi linamshikilia kiongozi wa kitengo cha vikosi vya usalama vilivyohusika katika mapigano ya usiku wa kuamkia leo na wanadhibiti hali hiyo.

Guinea-Bissau imekumbwa na mfululizo wa mapinduzi na majaribio ya mapinduzi tangu kupata uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1974
Guinea-Bissau imekumbwa na mfululizo wa mapinduzi na majaribio ya mapinduzi tangu kupata uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1974 REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Haya yamejiri baada ya makabiliano makali ya risasi kurupotiwa katika mji mkuu wa Guinea-Bissau mapema leo Ijumaa asubuhi baada ya walinzi wa vikosi maalum kwenda kuwatoa kizuizini waziri na kiongozi mwengine wa ngazi ya juu serikalini.

Walinzi hao wa kitaifa waliwachukua maofisa hao kabla ya kurejea kambini kusini mwa mji mkuu.

Kwa mujibu wa taarifa, vikosi maalum viliingilia kati baada ya mazungumzo ya kuwaachia huru kukwama, hatua ambayo ilisababisha kutokea kwa makabiliano ya risasi kabla ya hali ya utulivu kurejeshwa.

Waziri wa fedha, Souleiman Seidi, na katibu wa hazina kuu ya serikali, Antonio Monteiro, walikuwa wanazuiliwa wakati kukiwa na uchunguzi wa madai ya kutolewa kwa Dola milioni 10 ya fedha za serikali kwa njia isiyo ya kawaida.

Maofisa hao walihojiwa Alhamisi alasiri na uchunguzi kuanzishwa dhidi yao kubaini malipo kwa kampuni 11 yalivyofikiwa.

Guinea-Bissau imekumbwa na mfululizo wa mapinduzi na majaribio ya mapinduzi tangu kupata uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1974.

Mwezi Februari mwaka jana, rais alisema alinusurika jaribio la mapinduzi baada ya kuripotiwa kwa makabiliano ya risasi katika tukio ambalo watu 11 waliuawa.

Bila kutoa maelezo zaidi, alisema shambulio hilo linahusishwa na ulanguzi wa dawa za kulevya nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.