Pata taarifa kuu

ECOWAS imelaani machafuko yaliyotokea nchini  Guinea-Bissau

Jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imelaani vikali mapigano yalioripotiwa Ijumaa ya wiki hii nchini Guinea-Bissau, licha ya hali ya utulivu kuripotiwa kurejea leo Jumamosi.

ECOWAS imelaani vikali mapigano yalioripotiwa Ijumaa ya wiki hii nchini Guinea-Bissau
ECOWAS imelaani vikali mapigano yalioripotiwa Ijumaa ya wiki hii nchini Guinea-Bissau REUTERS - FRANCIS KOKOROKO
Matangazo ya kibiashara

Makabiliano kati ya maofisa wa ulinzi wa kitaifa na wale wa vikosi maalum vinavyotoa ulinzi wa rais, yalianza usiku wa Alhamis katika jiji kuu la nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu wawili.

Katika taarifa yake, ECOWAS imesema inalaani kwa kiasi kikubwa machafuko hayo na majaribio yoyote ya kuvuruga mpangilio wa kikatiba na utawala wa kisheria nchini Guinea-Bissau.

ECOWAS aidha imetoa wito wa kukamatwa na kushtakiwa kwa watu waliohusika na vurugu hizo ambazo mamlaka nchini humo zimesema zilikuwa jaribio la mapinduzi ya kijeshi.

Hali ya utulivu imeripotiwa kurejea nchini humo
Hali ya utulivu imeripotiwa kurejea nchini humo REUTERS - STRINGER

Hali ya utulivu ilirejea tena katika taifa hilo lenye historia ya kukosa udhabiti Ijumaa asubuhi baada ya jeshi kusema lilikuwa limemkata kanali Victor Tchongo,kamanda wa kikosi cha ulinzi wa kitaifa.

Wanachama wa kikosi cha ulinzi wa kitaifa siku ya Alhamis jioni, walitekeleza uvamizi katika kituo cha polisi wakiwa na lengo na kumtorosha waziri wa fedha Souleiman Seidi na katibu katika wizara hiyo Antonio Monteiro, kwa mujibu wa taarifa ya kiitelenjsia ya jeshi.

Maofisa hao wa serikali walikuwa wanahojiwa kutokana na hatua ya kuondoa Dolla milioni 10 kutoka katika akaunti za benki za serikali. Walikuwa wamezuiliwa kwa agizo la waendesha mashataka wa serikali, ambao wanateuliwa na rais.

ECOWAS aidha inatawaka waliohusika kuwajibishwa
ECOWAS aidha inatawaka waliohusika kuwajibishwa AFP - KOLA SULAIMON

Guinea-Bissau imekumbwa na mfululizo wa mapinduzi na majaribio ya mapinduzi tangu kupata uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1974.

Mwezi Februari mwaka jana, rais alisema alinusurika jaribio la mapinduzi baada ya kuripotiwa kwa makabiliano ya risasi katika tukio ambalo watu 11 waliuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.