Pata taarifa kuu

Gabon: Ali Bongo yuko 'huru' na anaweza kuondoka nchini, atangaza Jenerali Oligui

Haya yametangazwa katika taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa rais wa mpito iliyosomwa Jumatano hii jioni kwenye runinga ya taifa.

Rais wa Gabon Ali Bongo (kulia) akiwa katika Ikulu ya Rais mjini Libreville Machi 2, 2023.
Rais wa Gabon Ali Bongo (kulia) akiwa katika Ikulu ya Rais mjini Libreville Machi 2, 2023. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

 

Rais wa Gabon aliyeondolewa madarakani, Ali Bongo Ondimba, yuko "huru kufanya anachokitaka" na "anaweza kwenda nje ya nchi, ikiwa anataka," Kanali Ulrich Manfoumbi Manfoumbi ametangaza kwenye televisheni ya serikali, akisoma taarifa kwa vyombo vya habari "iliyotiwa saini" na Jenerali Oligui, ambaye sasa anaongoza taifa hilo.

Ali Bongo, madarakani kwa miaka 14, alikuwa chini ya kizuizi cha nyumbani tangu mapinduzi ya kijeshi ya Agosti 30, yaliyotekelezwa bila umwagaji damu chini ya saa moja baada ya kambi yake kutangaza kuchaguliwa kwake tena katika kura iliyoelezwa kuwa ya udanganyifu na viongozi wa mapinduzi.

“Kwa kuzingatia hali yake ya afya, aliyekuwa Rais wa Jamhuri Ali Bongo Ondimba yuko huru kufanya anachotaka. Anaweza, akipenda, kwenda nje ya nchi kufanya uchunguzi wake wa afya,” taarifa hiyo kwa vyombo vya habari imeongeza.

Ali Bongo alipatwa na kiharusi kibaya mnamo mwezi Oktoba 2018 ambacho kilimfanya adhoofike kimwili, huku mguu wake wa kulia na mkono hasa akivitumia kwa shida.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.