Pata taarifa kuu

Gabon: Brice Nguema aapishwa kama rais wa mpito

NAIROBI – Jenerali Brice Oligui Nguema ambaye aliongoza mapinduzi ya wiki iliyopita nchini Gabon, ameapishwa hivi leo kuwa rais wa mpito akiahidi kufanya uchaguzi wa huru na wazi punde tu kipindi cha mpito kitakapomalizika.

Kiongozi wa kijeshi nchini Gabon, Jenerali Brice Nguema akionekana huko Libreville mnamo Agsoti 16, 2023 wakati wa sherehe kuelekea siku ya uhuru. (Photo by AFP)
Kiongozi wa kijeshi nchini Gabon, Jenerali Brice Nguema akionekana huko Libreville mnamo Agsoti 16, 2023 wakati wa sherehe kuelekea siku ya uhuru. (Photo by AFP) © AFP
Matangazo ya kibiashara

Jumatano iliyopita, Nguema aliongoza wanajeshi wengine katika kumpindua rais Ali Bongo Ondimba, na kuangusha utawala wa familia hiyo wa takriban miaka 55.

Mapinduzi hayo yalikuja punde tu baada ya Bongo mwenye umri wa miaka 64, kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa mwishoni mwa mwezi uliopita.

Akiwa amevalia mavazi mekundu ya sherehe ya Walinzi wa Republican, Nguema pia ameapa kuhifadhi kile ameita mafanikio ya demokrasia, katika hafla hiyo iliyofanywa mbele ya majaji wa Mahakama ya Kikatiba.

Ijumaa ya Agosti 1, aliahidi kuunda taasisi zaidi za kidemkrasia ambazo zinaheshimu haki za kibinadamu .

Baadhi ya mataifa na mashirika ya magharibi, yamelaani mapinduzi hayo, japo yanakiri uchaguzi haukuwa wa huru na haki haswa ikizingatiwa kuwa huduma za intaneti zilifungwa na kafyu kutangazwa siku ya Jumamosi.

Kikawaida, mapinduzi ya kijeshi sio suluhisho, lakini lazima tukumbuke kuwa nchini Gabon, uchaguzi ulikumbwa na dosari chungu nzima. Alisema mkuu wa sera za kigeni wa umoja wa Ulaya Josep Borrell.

Rais Bongo alikuwa anatafuta kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu, baada ya kuingia madarakani mwaka 2009 kufuatia kifo cha babake Omar, ambaye aliongoza nchi  hiyo kwa mkono wa chuma kwa zaidi ya miaka 40.

Mataifa matano nchini Afrika yamepitia mapinduzi ya kijeshi yakiwemo Mali, Guinea, Sudan, Burkina Faso na Niger katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.