Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Gabon: Utawala wa kijeshi wafungua tena mipaka

Wanajeshi waliopindua Ali Bongo Ondimba nchini Gabon siku ya Jumatano wametangaza kufungua tena mipaka ya nchi kavu, angani na baharini leo Jumamosi, Kanali Ulrich Manfoumbi Manfoumbi, msemaji wa Kamati ya Mpito na Amani, ametangaza kwenye televisheni ya taifa.

Kanali Ulrich Manfoumbi Manfoumbi, msemaji wa Kamati ya Mpito na Amani (CTRI), akitangaza kufunguliwa tena kwa mipaka ya nchi kavu baharini na angani, nchini Gabon.
Kanali Ulrich Manfoumbi Manfoumbi, msemaji wa Kamati ya Mpito na Amani (CTRI), akitangaza kufunguliwa tena kwa mipaka ya nchi kavu baharini na angani, nchini Gabon. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

"Tuna nia ya kuhifadhi heshima ya utawala wa sheria, uhusiano mzuri na majirani zetu na nchi zote ulimwenguni, na ili kukuza mwendelezo wa serikali, huku tukionyesha nia yetu thabiti ya kutimiza ahadi zetu za kimataifa", CTRI "inaamua kufungua tena mipaka ya nchi kavu, baharini na angani” kuanzia Jumamosi. 

Mipaka hii ilikuwa imefungwa tangu mapinduzi yaliyomng'oa mamlakani Ali Bongo, ambaye alitawala nchi hiyo kwa miaka 14, baada ya babake kuitawala kwa mkono wa chuma kwa miaka 41.

Hayo yanajiri wakati Ufaransa imetangaza kusitisha ushirikiano wa kijeshi na utawala mpya nchini Gabon.

Waziri wa Majeshi ya Ufaransa Sebastien Lecornu amesema kuwa Paris imesitisha ushirikiano wa kijeshi na utawala mpya nchini Gabon. Haya yanajiri huku kiongozi Jenerali Brice Oligui Nguema akiapa kuwa taasisi za nchi zitakuwa za kidemokrasia zaidi, siku mbili baada ya kuongoza mapinduzi yaliyomaliza miaka 55 ya utawala wa familia ya Bongo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.