Pata taarifa kuu
MAPINDUZI-USALAMA

Gabon: Mfahamu Jenerali Brice Oligui Nguema, aliyetangazwa na jeshi kuwa rais wa mpito

Wanajeshi ambao "walifanya mapinduzi" nchini Gabon mnamo Agosti 30, 2023, kwa kumtimua mamlakani rais aliyetangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais mapema siku ya Jumatano, Ali Bongo Ondimba, walimtatangaza Jumatano jioni Mkuu wa kikosi cha walinzi wa jamhuri, Jenerali Brice Oligui Nguema kuwa rais wa mpito. Afisa wa ngazi ya juu ambaye amekuwa karibu na rais kwa muda mrefu.

Video hii iliyonaswa na Gabon 24 mnamo Agosti 30, 2023 inaonyesha wanajeshi wa Gabon wakiwa wamembeba Jenerali Brice Oligui Nguema (katikati), mkuu wa kikosi cha walinzi wa rais Ali Bongo Ondimba
Video hii iliyonaswa na Gabon 24 mnamo Agosti 30, 2023 inaonyesha wanajeshi wa Gabon wakiwa wamembeba Jenerali Brice Oligui Nguema (katikati), mkuu wa kikosi cha walinzi wa rais Ali Bongo Ondimba AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Jenerali Oligui Nguema alichukua mamlaka Gabon mnamo Agosti 30, 2023. Ni afisa wa ngazi ya juu ambaye amekuwa karibu na rais kwa muda mrefu tangu hata kabla ya kifo cha Albert-Bernard Bongo (Omar Bongo), babakr rais Ali Bongo.

Jenerali Brice Clotaire Oligui Nguema, mtoto wa aliyekuwa afisa jeshini, alifunzwa nchini Morocco, nchi iliyo karibu sana na Gabon, kabla ya kuwa msaidizi wa kambi ya Al Haj Omar Bongo, rais wa Gabon kuanzia mwaka 1967 hadi 2009. Brice Clotaire Oligui Nguema alibakia kweye nafasi hiyo hadi kifo cha rais al Haj Omar Bongo mnamo mwezi Juni 2009. Ali Bongo alimrithi babake lakini kazi ya afisa huyo ikabadilika. Alitumwa nje ya nchi, kama mshirika wa kijeshi katika ubalozi wa Gabon nchini Morocco na kisha Senegal. Hatua ambayo Brice Clotaire Oligui Nguema aliipokea shingo upande, na hivyo kuhisi kama uhamisho wa kulazimishwa, duru za kuaminika zimebaini.

"Inafahamika kwamba, Ali Bongo alipochaguliwa, kulikuwa na migogoro kati yake na Jenerali Oligui," anasema Florence Bernault, profesa na mtafiti katika Kituo cha Historia ya Sayansi, mwanahistoria na mtaalamu katika Afrika ya Kati. Hivyo aliteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali za kidiplomasia kwa muda kidogo kuanzia mwaka 2009.”

Bergès Mietté, mtafiti katika maabara ya Afrika duniani, anathibitisha kwa upande wake: “Baada ya Ali Bongo kuingia madarakani, Brice Oligui Nguema alishutumiwa kushiriki katika jaribio la mapinduzi lililopangwa na Jenerali Ntumpa [mwaka 2009]. Lakini isipokuwa kwamba jukumu lake katika mapinduzi haya lilikuwa halijathibitishwa wakati wa kesi iliyosikilizwa katika mahakam ya jijeshi mjini Libreville. Tangu wakati huo alifukuzwa kwenye wadhifa wake, na kutumwa katika ubalozi wa Gabon nchini Senegal, kama afisa anayehusika na masuala ya kijeshi. "

Alirejeshwa Libreville baada ya rais Ali Bongo kupatwa ugonjwa wa Kiharusi

Miaka kumi baadaye, baada ya rais Ali Bongo kupatwa ugonjwa wa Kiharusi, Brice Clotaire Oligui Nguema, wakati huo alikuwa na cheo cha kanali, alirejea nchini na kuwa kwenye mstari wa mbele. Alichukua nafasi ya Frédéric Bongo, kaka wa kambo wa rais, kama mkuu wa upelelezi wa kikosi cha walinzi wa jamhuri.

Mnamo mwaka 2020, iligundulika kuwa wanajeshi wana uwezo mkubwa wa kifedha: uchunguzi wa Organized Crime and Corruption Reporting Project, kundi la wachunguzi, lilibaini kuwa Brice Clotaire Oligui Nguema anamiliki mali kadhaa nchini Marekani, za jumla ya thamani ya dola milioni moja. Mnamo mwaka 2018, kwa mfano, alilipa dola 447,000 taslimu ili kununua nyumba katika jiji la Silver Spring.

Miezi sita baada ya kurejea kutoka nje ya nchi, aliteuliwa kuwa mkuu wa kikosi cha walinzi wa jamhuri ambapo aliimarisha mfumo wa ulinzi kwa mkuu wa nchi. Dhamira yake ilikuwa kuongoza kikosi cha walinzi kambi inayomlinda Ali Bongo. Na siku ya Jumatano Agosti 30, 2023 aliamua kuangusha utawala wa mshirika wake wa karibu.

Kwenye Gazeti la Le Monde, alisema mapema siku ya Jumatano: "Unajua kwamba nchini Gabon kuna malalamiko mengi na watu wengi wangi wakinungunika kutokana na utawala, mbali na kunungunika huku, rais Ali Bongo ana ugonjwa wa muda mrefu. Kila mtu anazungumza juu yake, lakini hakuna mtu anayechukua jukumu. Hakuwa na haki ya kuhudumu kwa muhula wa tatu, Katiba ilivunjwa, utaratibu wa uchaguzi wenyewe haukuwa mzuri. Kwa hiyo jeshi liliamua kufungua ukurasa mpya, kuchukua majukumu yake. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.