Pata taarifa kuu
MAPANDUZI-USALAMA

Mapinduzi nchini Gabon: Jenerali Brice Oligui Nguema ateuliwa kuwa 'rais wa mpito'

Nchini Gabon, Jenerali Brice Oligui Nguema ameteuliwa na wanajeshi waliofanya mapinduzi kuwa "rais wa mpito". Ali Bongo ambaye ametimyliwa mamlakani kupitia mapinduzi, amewekwa chini ya kifungo cha nyumbani, viongozi wa mapinduzi wametangaza kwenye televisheni mnamo Agosti 30, 2023. Mmoja wa watoto wa rais Bongo, Noureddin Bongo Valentin, pia amekamatwa.

Video hii iliyonaswa na Gabon 24 mnamo Agosti 30, 2023 inaonyesha wanajeshi wa Gabon wakiwa wamembeba Jenerali Brice Oligui Nguema (katikati), mkuu wa kikosi cha walinzi wa rais Ali Bongo Ondimba.
Video hii iliyonaswa na Gabon 24 mnamo Agosti 30, 2023 inaonyesha wanajeshi wa Gabon wakiwa wamembeba Jenerali Brice Oligui Nguema (katikati), mkuu wa kikosi cha walinzi wa rais Ali Bongo Ondimba. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Taarifa imesomwa kwenye televisheni ya Gabon 24. "Jenerali Oligui Nguema Brice ameteuliwa kwa kauli moja kuwa rais wa Kamati ya Mpito na Marejesho ya Taasisi," afisa mmoja ametangaza mbele ya makumi ya maafisa wakuu na majenerali, ambao wanawakilisha vikosi vyote vya jeshi la Gabon.

Jenerali Brice Oligui Nguema alikuwa, kabla ya mapinduzi, kamanda mkuu wa kikosi cha walinzi wa taifa, kitengo cha wasomi wa jeshi la Gabon. Mtoto wa afisa, aliyefunzwa katika Chuo cha Kijeshi cha Kifalme cha Meknes huko Morocco, alikuwa hata mmoja wa wasaidizi wa kambi ya Omar Bongo, rais wa zamani na baba wa mkuu wa sasa wa nchi, na hii, hadi kifo chake Juni 2009.

Picha hii ya video iliyochukuliwa kutoka kwa video iliyotolewa na na AFPTV kutoka Gabon 24 Agosti 30, 2023 inamuonyesha Kanali Ulrich Manfoumbi Manfoumbi (katikati), msemaji wa Kamati ya Mpito na Marejesho ya Taasisi (CTRI), akisoma taarifa kwenye televisheni.
Picha hii ya video iliyochukuliwa kutoka kwa video iliyotolewa na na AFPTV kutoka Gabon 24 Agosti 30, 2023 inamuonyesha Kanali Ulrich Manfoumbi Manfoumbi (katikati), msemaji wa Kamati ya Mpito na Marejesho ya Taasisi (CTRI), akisoma taarifa kwenye televisheni. AFP - -

Muda wa mpito wa jeshi kuingia madarakani haujabainishwa. Viongozi wa mapinduzi wanadumisha sheria ya kutotoka nje "hadi utakapochukuliwa uamuzi mwingine". Sheria hii ya kutotoka nje ilitangazwa siku nne zilizopita na mamlaka ya rais aliyeondolewa "kulinda utulivu". "Kuanzia kesho, Wagabon wataweza tena kufanya shughuli zao kwa uhuru kati ya saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni. 

Kanali Ulrich Manfoumbi Manfoumbi pia ametangaza kurejeshwa kwa matangazo ya vyombo vya habari yaliyositishwa Jumamosi jioni, siku ya uchaguzi wa rais. "Marufuku hii ya muda ya matangazo" ililenga vyombo vya habari vinavyozungumza Kifaransa pekee: France 24, RFI na TV5 Monde.

Sasa, kwa mujibu wa kundi la vikosi vya usalama vya Gabon vilivyoasi vilivyozungumza kwenye televisheni ya taifa mapema Jumatano, yuko chini ya kifungo cha nyumbani, akishutumiwa kwa "utawala usiotabirika, usiowajibika."

Askari hao wanaodai kutwaa mamlaka wamesema watu wa karibu na Bongo wamekamatwa kwa "usaliti mkubwa," ubadhirifu na ufisadi, ingawa haikujulikana kama rais mwenyewe alikabiliwa na mashtaka hayo.

Kwa mujibu wa kundi la vikosi vya usalama vya Gabon vilivyoasi vilivyozungumza kwenye televisheni ya taifa mapema Jumatano, Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba yuko chini ya kifungo cha nyumbani, akishutumiwa kwa "utawala usiotabirika, usiowajibika."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.