Pata taarifa kuu

Raia wa Gabon wanapiga kura kuwachagua viongozi wapya

Nairobi – Raia wa Gabon wanapiga kura kumchagua rais, wabunge na wawakilishi wa manispaa. 

Uchaguzi mkuu unaendelea nchini Gabon
Uchaguzi mkuu unaendelea nchini Gabon REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Rais Ali Bongo, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2009, baada ya kifo cha baba yake Omar Bongo, aliyeongoza kwa miaka 42 tangu 1967 anawania tena. 

Bongo na mpinzani wake mkuu Albert Ondo Ossa wanaongoza kinyang'anyiro cha wagombea 14 wanaowania nafasi ya juu katika taifa hilo ndogo  la Afrika ya kati lenye utajiri wa mafuta.

Onda Ossa, profesa wa uchumi mwenye umri wa miaka 69 ambaye aliwahi kuwa waziri chini ya Bongo kutoka 2006 hadi 2009, alichaguliwa na mrengo wa upinzani kama mgombea wake mkuu pamoja siku nane tu kabla ya uchaguzi.

Rais Ali Bongo analenga kuongoza taifa hilo kwa muhula wa tatu
Rais Ali Bongo analenga kuongoza taifa hilo kwa muhula wa tatu REUTERS - STRINGER

Bongo anatafuta muhula mwingine wa miaka saba, baada ya mwaka 2016 alipata ushindi mwembamba kwa kumshinda mpinzani wake Jean Ping kwa kura 5,500.

Kuelekea uchaguzi huu, Bongo amekuwa akisumbuliwa na changamoto ya kiafya baada ya kupata kiharusi Oktoba mwaka 2018, na kutoonekana kwa muda miezi 10. 

Mwezi Januari mwaka 2019, alikabiliwa na jaribio la jeshi kutaka kumwondoa madarakani. 

Bongo na mpinzani wake mkuu Albert Ondo Ossa wanaongoza kinyang'anyiro cha wagombea 14 wanaowania nafasi ya juu katika taifa hilo ndogo  la Afrika ya kati lenye utajiri wa mafuta.
Bongo na mpinzani wake mkuu Albert Ondo Ossa wanaongoza kinyang'anyiro cha wagombea 14 wanaowania nafasi ya juu katika taifa hilo ndogo  la Afrika ya kati lenye utajiri wa mafuta. AFP - LUDOVIC MARIN,STEEVE JORDAN

Anawania kwa muhula wa tatu, akikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Albert Ondo Ossa, anayeungwa mkono na vyama sita vya upinzani. 

Kuna wagombea wengine 12, lakini hawana umaarufu. Wachambuzi wa siasa wanatabiri kuwa rais Bongo, atatangazwa mshindi kwenye uchaguzi huo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.